-
Uko Macho Kuelekea Nyakati Zetu?Mnara wa Mlinzi—1998 | Septemba 15
-
-
Uko Macho Kuelekea Nyakati Zetu?
KUWA macho kuelekea hatari kwaweza kufanyiza tofauti kati ya uhai na kifo. Hili laweza kutolewa kielezi na lililotukia katika visiwa viwili vya volkano.
Mlima Pelée, volkano yenye kufisha zaidi ya karne ya 20, ulilipuka Mei 8, 1902, katika kisiwa cha Karibea cha Martinique. Mlipuko huo uliua karibu idadi ya wakazi wote 30,000 wa Saint Pierre, jiji lililo karibu na volkano.
Katika Juni 1991, Mlima Pinatubo ulilipuka labda ukiwa mlipuko mkubwa zaidi katika karne hii. Ulitokea katika eneo la Filipino lenye idadi kubwa ya watu nao ulisababisha vifo vya watu 900 hivi. Hata hivyo, wakati huu mambo mawili yalisaidia kuokoa maelfu ya watu: (1) kuwa macho kuelekea hatari hiyo na (2) utayari wa kutenda kupatana na maonyo.
Tendo Lifaalo Liliokoa Uhai
Mlima Pinatubo ulikuwa umekuwa bwete kwa maelfu ya miaka wakati katika Aprili 1991, ulianza kutoa dalili za mlipuko uliokuwa ukikaribia. Mvuke na salfa dioksidi ilianza kuvuja kwenye kilele. Wakazi wa mahali hapo walihisi mfululizo wa mitetemeko midogo ya dunia, na kuba ya lava iliyoganda ambayo iliashiria msiba, ilianza kuibuka kutoka kwenye mlima. Wanasayansi kutoka Taasisi ya Sayansi ya Volkano na Mitetemeko ya Dunia ya Filipino walikesha sana na hatimaye wakawasadikisha wakuu wa serikali kwamba lingekuwa jambo la hekima kuhamisha wakazi 35,000 kutoka majiji na vijiji vilivyo karibu na hapo.
Yaeleweka kwamba watu husita kuhama nyumba zao bila sababu, lakini kusitasita kulishindwa kwa wonyesho wa vidio ulioonyesha waziwazi hatari za mlipuko wa volkano. Watu wengi waliotoka walifanya hivyo kwa wakati ufaao. Siku mbili baada ya hapo, mlipuko mkubwa zaidi ulivurumisha majivu umbali wa kilometa mchemraba nane angani. Baadaye mitiririko ya matope iliua mamia ya watu. Hata hivyo, labda maelfu waliokoka, kwa sababu watu walikuwa wametahadharishwa kuhusu hatari hiyo nao wakatii maonyo.
Kuponyoka Maafa Makubwa Yaliyotokezwa na Binadamu
Katika karne ya kwanza ya Wakati wetu wa Kawaida, Wakristo waliokuwa wakiishi Yerusalemu pia iliwabidi kuamua kama wangeyaacha makao yao. Kukimbia kutoka katika jiji hilo mwaka wa 66 W.K. kuliwaokoa na uharibifu ambao uliwapata wakazi wale wengine na maelfu ya Wayahudi ambao walikuwa wamekuja Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Kupitwa ya mwaka wa 70 W.K. Watu zaidi ya milioni moja walikuwa ndani ya jiji hilo lenye kuta wakiadhimisha Sikukuu ya Kupitwa wakati jeshi la Roma lilipofanya isiwezekane kabisa kupata fursa ya kutoroka. Njaa kuu, kung’ang’ania mamlaka, na mashambulizi yenye ukatili ya Waroma yalitokeza vifo vya watu zaidi ya milioni moja.
Maafa makubwa yaliyokomesha maasi ya Wayahudi dhidi ya Waroma hayakuja bila kutangazwa. Miongo kadhaa mapema, Yesu Kristo alikuwa ametabiri kwamba Yerusalemu lingezingirwa. Yeye alisema hivi: “Wakati mwonapo Yerusalemu limezingirwa na majeshi yaliyopiga kambi, ndipo jueni kwamba kufanywa ukiwa kwalo kumekaribia. Ndipo waacheni wale walio katika Yudea waanze kukimbia hadi kwenye milima, na waacheni wale walio katikati yalo waondoke, na waacheni wale walio katika sehemu za mashambani wasiingie ndani yalo.” (Luka 21:20, 21) Maagizo hayo yalikuwa wazi, na wafuasi wa Yesu waliyachukua kwa uzito.
Mwanahistoria wa karne ya nne Eusebia Kaisaria aripoti kwamba Wakristo wa Yudea yote walitenda kulingana na onyo la Yesu. Waroma walipoacha kuzingira Yerusalemu kwa mara ya kwanza katika 66 W.K., Wakristo wengi Wayahudi walienda kuishi katika jiji la Wasio Wayahudi la Pella, katika mkoa wa Roma wa Perea. Kwa kuwa macho kuelekea nyakati zao na kutenda kulingana na onyo la Yesu, waliponyoka kule ambako kumeitwa “mojawapo ya kuzingira kwenye kuogofya zaidi katika historia yote.”
Leo, uangalifu huohuo wahitajiwa. Na ndivyo ilivyo kutenda kihususa. Makala ifuatayo itaeleza sababu ya hilo.
-
-
Ni Saa ya Kuamka!Mnara wa Mlinzi—1998 | Septemba 15
-
-
Ni Saa ya Kuamka!
“USIKOSEE kuhusu kizazi tunamoishi; kwetu sisi tayari ni saa ya kuamka kutoka usingizini.” (Waroma 13:11, Knox) Mtume Paulo aliandikia Wakristo katika Roma maneno hayo yapata miaka 14 kabla ya msiba mkuu wa mfumo wa mambo wa Kiyahudi katika 70 W.K. Kwa sababu walikuwa macho kiroho, Wakristo Wayahudi hawakuwa Yerusalemu wakati huo wenye hatari, hivyo waliponyoka kifo au utumwa. Lakini walijuaje kwamba walihitaji kuondoka katika jiji hilo bila kuingia humo tena?
Yesu Kristo alikuwa ameonya kwamba adui zao wangezingira Yerusalemu na kwamba wakazi wake wangeangamizwa kabisa. (Luka 19:43, 44) Baada ya hapo, Yesu aliwapa wafuasi wake waaminifu ishara yenye mambo mengi ambayo haikuwa ngumu kuitambua. (Luka 21:7-24) Kuhusu wale Wakristo walioishi Yerusalemu, kuacha jiji hilo kulimaanisha kuacha makao yao na kazi zao. Hata hivyo, uangalifu wao na kukimbia kwao kuliokoa uhai wao.
Yesu alipotabiri juu ya uharibifu wa Yerusalemu, wanafunzi wake walimuuliza hivi: “Ni wakati gani mambo haya yatakuwa, nayo itakuwa ni nini ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo?” (Mathayo 24:3) Katika kujibu kwake, Yesu alilinganisha kuwapo kwake kwa wakati ujao na kipindi kilichoongoza hadi kwenye Furiko la tufeni pote la siku za Noa. Yesu alionyesha kwamba Gharika ilimaliza watu waovu wote. (Mathayo 24:21, 37-39) Hivyo alionyesha kwamba Mungu angeingilia kati mambo ya binadamu tena. Kwa kadiri gani? Naam, kufikia hatua ya kuondoa ulimwengu au mfumo wote wa mambo ulio mwovu! (Linganisha 2 Petro 3:5, 6.) Je, hilo lingetokea wakati wetu?
Je, Mambo Yote Yanaendelea Sawasawa?
Wayahudi wengi wa karne ya kwanza hawakuwazia wakati wowote kwamba jiji lao takatifu Yerusalemu, lingeweza kuharibiwa. Kutoamini kama huko mara nyingi kumeenea miongoni mwa watu wanaoishi karibu na volkano lakini hawajapata kamwe kuona moja ikilipuka. “Haiwezekani katika maisha yangu” ndilo jibu la kawaida wakati maonyo yatolewapo. “Volkano halisi hulipuka baada ya kila karne mbili au tatu,” aeleza mwanasayansi wa volkano Lionel Wilson. “Unakuwa na wasiwasi ikiwa wazazi wako walilazimika kuhama kwa sababu ya mlipuko. Lakini kama uliwapata wazakuu wako, basi hiyo ni hadithi tu.”
Hata hivyo, habari iliyo sahihi yaweza kutuwezesha kutambua dalili za hatari na tuzichukue kwa uzito. Kati ya wale waliokimbia kutoka Mlima Pelée, mmoja alikuwa anafahamu volkano na kuzielewa dalili za hatari. Ishara hizo pia zilielezwa kwa usahihi muda mfupi baada ya mlipuko wa Mlima Pinatubo. Wanasayansi wa volkano ambao walichunguza kani zisizoonekana zikiongezeka polepole ndani ya mlima walisadikisha watu wa mahali hapo waondoke sehemu hiyo.
Bila shaka, sikuzote watu fulani watapuuza ishara za hatari na kusisitiza kwamba hakuna kitu kitakachotendeka. Huenda hata wakadhihaki wale wenye kuchukua hatua yenye kukata maneno. Mtume Petro alitabiri kwamba maoni kama hayo yangekuwa ya kawaida katika siku yetu. “Mwajua hili kwanza,” akasema, “kwamba katika siku za mwisho watakuja wadhihaki pamoja na dhihaka zao, wakiendelea kulingana na tamaa zao wenyewe na kusema: ‘Kuko wapi kuwapo kwake huku kulikoahidiwa? Kwani, kutoka siku baba zetu wa zamani walipolala katika kifo, mambo yote yanaendelea sawasawa kabisa kama kutoka mwanzo wa kuumba.’”—2 Petro 3:3, 4.
Je, waamini kwamba twaishi katika “siku za mwisho?” Katika kichapo The Columbia History of the World, John A. Garraty na Peter Gay wauliza: “Je, twaona ustaarabu wetu ukiharibika?” Basi hawa wanahistoria huchunguza matatizo ya serikali, kuongezeka kwa uhalifu tufeni pote na maasi dhidi ya serikali, kuharibika kwa maisha ya familia, kushindwa kwa sayansi na tekinolojia kutatua matatizo ya jamii, matatizo ya mamlaka, na kuzorota kwa maadili na kidini ulimwenguni pote. Wao wamalizia hivi: “Kama hizi si ishara za mwisho halisi, zaonekana isivyo kawaida kuwa hivyo.”
Tuna sababu nzuri ya kuamini kwamba “mwisho” uko karibu. Hatupaswi kuhofu mwisho wa tufe la dunia yenyewe, kwa kuwa Biblia husema kwamba Mungu ‘aliiweka nchi juu ya misingi yake, isitikisike milele.’ (Zaburi 104:5) Lakini, twapaswa kutazamia mwisho wa mapema wa mfumo wa mambo ambao umesababishia wanadamu taabu nyingi sana. Kwa nini? Kwa sababu twaweza kuona sehemu nyingi zilizo dhahiri zinazotambulisha siku za mwisho wa mfumo huu, kama ilivyotajwa na Yesu Kristo. (Ona sanduku “Baadhi ya Sehemu za Siku za Mwisho.”) Kwa nini usilinganishe maneno ya Yesu na matukio ya ulimwengu? Kufanya hivyo, huenda kukakusaidia ufanye maamuzi yako mwenyewe na ya familia yako. Lakini kwa nini uchukue hatua sasa hivi?
Uhitaji Halisi wa Kubaki Macho
Ingawa wanasayansi huenda wakajua mlipuko wa volkano ukaribiapo, hawawezi kujua hasa utakapotokea. Vivyo hivyo, kuhusu mwisho wa huu mfumo wa mambo, Yesu alisema: “Kuhusu siku hiyo na saa hiyo hakuna mtu ajuaye, wala hao malaika wa mbingu wala Mwana, ila Baba tu.” (Mathayo 24:36) Kwa kuwa hatujui hasa wakati mfumo wa mambo utakapokoma, Yesu alitupatia onyo hili: “Jueni jambo moja, kwamba ikiwa mwenye nyumba angalijua ni katika lindo gani mwizi anakuja, angalifuliza kuwa macho na hangaliruhusu nyumba yake ivunjwe na kuingiwa. Kwa sababu hiyo nyinyi pia jithibitisheni wenyewe kuwa tayari, kwa sababu kwenye saa msiyoifikiri kuwa hiyo, Mwana wa binadamu [Yesu] anakuja.”—Mathayo 24:43, 44.
Maneno ya Yesu yaonyesha kwamba mwisho wenye msiba mkuu wa mfumo huu utaupata ulimwengu huu bila kutazamia. Hata kama sisi ni wafuasi wake, twahitaji ‘kujithibitisha wenyewe kuwa tayari.’ Hali yetu ni kama ile ya mwenye nyumba ambaye huenda akapatwa bila kutazamia kwa sababu hujui ni lini mwizi atakapovunja nyumba yake.
Vivyo hivyo, mtume Paulo aliwaambia Wakristo katika Thesalonike hivi: “Nyinyi wenyewe mwajua vema kabisa kwamba siku ya Yehova inakuja sawasawa kabisa na mwizi usiku. . . . Akina ndugu, hamumo katika giza, hivi kwamba siku hiyo iwafikie nyinyi ghafula kama vile ingekuwa kwa wezi.” Paulo alisihi hivi pia: “Acheni tusiendelee kulala usingizi kama wengine, bali acheni tukae macho na kutunza hisi zetu.” (1 Wathesalonike 5:2, 4, 6, kielezi-chini katika New World Translation—With References) “Kukaa macho na kutunza hisi zetu” kwamaanisha nini?
Tofauti na kukimbia kwa Wakristo wa karne ya kwanza kutoka Yerusalemu, kukimbilia kwetu usalama hakuhusishi kuondoka katika jiji fulani. Baada ya kuhimiza waamini wenzake katika Roma waamke kutoka usingizini, Paulo aliwasihi ‘waondoe kazi za giza’ na ‘kumvaa Bwana Yesu Kristo.’ (Waroma 13:12, 14) Kwa kufuata hatua za Yesu kwa ukaribu, tutakuwa macho kuelekea nyakati hizi, na uangalifu huu wa kiroho utafanya iwezekane kwetu kupokea ulinzi wa kimungu wakati mfumo huu mwovu wa mambo ukomapo.—1 Petro 2:21.
Wale ambao hufuata Yesu Kristo hufurahia maisha yenye maana na yenye kuridhisha. Mamilioni ya Mashahidi wa Yehova wamegundua kwamba nira ya uanafunzi wa Kikristo ni yenye fadhili na yenye kuburudisha. (Mathayo 11:29, 30, kielezi-chini katika New World Translation—With References) Hatua ya kwanza ya kuwa mwanafunzi ni ‘kutwaa ujuzi juu ya Mungu na juu ya yule aliyemtuma, Yesu Kristo.’ (Yohana 17:3) Mashahidi hutembelea mamilioni ya nyumba kila juma ili kusaidia watu wapate “ujuzi sahihi wa kweli.” (1 Timotheo 2:4) Wangependezwa kujifunza Biblia nawe nyumbani mwako bila malipo. Na ukuapo katika ujuzi wa Neno la Mungu, bila shaka utasadikishwa kwamba siku zetu ziko tofauti. Kwa kweli ni saa ya kuamka kutoka usingizini!
-