-
Mtegemee Yehova Ili Kupata FarajaMnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
-
-
19. Kwa nini Paulo aliendelea na safari kutoka Troa hadi Makedonia, naye alipataje kitulizo hatimaye?
19 Alipokuwako Efeso, zaidi ya kuwaandikia ndugu katika Korintho, Paulo alimtuma Tito awasaidie, akimpa utume wa kuripoti juu ya itikio lao kwa ile barua. Paulo alitumaini kumkuta Tito, Troa. Huko Paulo alibarikiwa kwa fursa nzuri za kufanya wanafunzi. Lakini hilo halikumwondolea hangaiko lake kwa sababu Tito hakuwa amefika bado. (2 Wakorintho 2:12, 13) Kwa hiyo, akaendelea na safari kuelekea Makedonia, akitumainia kukutana na Tito huko. Hali ya kuhangaika ya Paulo iliongezwa na upinzani mwingi dhidi ya huduma yake. “Tulipokuwa tumefika Makedonia,” aeleza, “miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu. Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito.” (2 Wakorintho 7:5, 6) Kilikuwa kitulizo kama nini Tito alipofika mwishowe ili kumwambia Paulo juu ya itikio chanya la Wakorintho kwa barua yake!
20. (a) Kama ilivyokuwa katika kisa cha Paulo, ni ipi njia nyingine ya maana ambayo kwayo Yehova hupa faraja? (b) Ni nini kitakachochunguzwa katika makala inayofuata?
20 Mambo aliyojionea Paulo hufariji watumishi wa Mungu leo, ambao wengi wao hukabili majaribu ambayo huwafanya wawe “wanyonge” au “washuke moyo.” (Phillips) Ndiyo, ‘Mungu apaye faraja’ hujua mahitaji yetu mmoja-mmoja naye aweza kututumia tufarijiane, kama vile Paulo alivyopata faraja kupitia ripoti ya Tito juu ya mwelekeo wa kutubu wa Wakorintho. (2 Wakorintho 7:11-13) Katika makala yetu inayofuata, tutachunguza itikio changamfu la Paulo kwa Wakorintho na jinsi liwezavyo kutusaidia tuwe washiriki wenye matokeo wa faraja ya Mungu leo.
-
-
Mtegemee Yehova Ili Kupata FarajaMnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
-
-
Paulo alipata faraja kubwa kupitia ripoti ya Tito juu ya Wakorintho
-