Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marafiki wa Mungu Katika Visiwa vya Tonga
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
    • Mashua Quest Ilitumiwa Kutafuta Wanaopendezwa

      Miezi michache baada ya Ukumbusho wa mwaka wa 2002, mashua nyingine ilileta vitu vyenye thamani kwenye kisiwa cha mbali cha Ha’apai. Mashua hiyo ya meta 18 iliyoitwa Quest ilisafiri kutoka New Zealand hadi kwenye visiwa vya Tonga. Kati ya abiria kulikuwa na Gary na Hetty, pamoja na binti yao Katie. Ndugu na dada tisa wa Tonga pamoja na wamishonari wawili waliambatana nao mara mbili. Mashahidi wenyeji walisaidia kuendesha mashua hiyo kwa ustadi, nyakati nyingine katikati ya miamba wasiyoijua. Safari hizo hazikuwa zenye kustarehesha. Waliokuwa ndani ya mashua hiyo walikuwa wamekuja kufundisha kweli za Biblia. Walizunguka eneo kubwa la bahari wakitembelea visiwa 14. Habari njema ya Ufalme haikuwa imewahi kuhubiriwa katika baadhi ya visiwa hivyo.

      Watu waliitikiaje? Kwa ujumla, wahubiri hao wa baharini walikaribishwa kwa uchangamfu, kwa ukarimu, na pia kwa udadisi kama ilivyo desturi ya watu wa visiwani. Wenyeji wa visiwani walipoelewa kusudi la ziara hiyo, walithamini sana. Ilikuwa wazi kwa Mashahidi hao wageni kwamba watu wa kisiwa hicho waliliheshimu Neno la Mungu na walitambua uhitaji wao wa kiroho.—Mathayo 5:3.

      Mara nyingi, wageni walikaa chini ya miti inayokua katika maeneo yenye joto wakiwa wamezungukwa na watu ambao walikuwa na maswali mengi kuhusu Biblia. Kulipokuwa usiku, mazungumzo ya Biblia yaliendelea ndani ya nyumba za watu. Wenyeji wa kisiwa kimoja waliwasihi hivi Mashahidi waliokuwa wakiondoka: “Msiende! Mkiondoka ni nani watajibu maswali yetu?” Shahidi mmoja alisema: “Ilikuwa vigumu kuacha watu hao wengi wenye mfano wa kondoo ambao walikuwa na njaa ya kweli. Mbegu nyingi za kweli zimepandwa.” Mashua Quest ilipofika kwenye kisiwa kimoja, Mashahidi walimkuta kila mtu amevalia mavazi ya maombolezo. Mke wa afisa wa mji huo alikuwa amekufa muda mfupi tu kabla ya hapo. Afisa huyo aliwashukuru akina ndugu kwa kuleta ujumbe wa faraja kutoka katika Biblia.

      Haikuwa rahisi kufika kwenye visiwa fulani. Hetty anaeleza: “Kisiwa kimoja hakikuwa na nchi kavu ila tu miamba iliyochomoza kutoka baharini yenye urefu wa meta moja hivi. Tungeweza kufika kwenye kisiwa hicho kwa kutumia mtumbwi wa mpira. Kwanza, ilitubidi kuwatupia mikoba yetu watu wengi waliokuwa ufuoni tayari kuipokea. Kisha, mtumbwi huo ulipopanda juu ya mwamba ilitubidi turuke kabla haujateremka tena baharini.”

      Hata hivyo, si abiria wote waliokuwa wana-bahari stadi. Baada ya kusafiri kwa muda wa majuma mawili, nahodha aliandika hivi kuhusu safari ya kurudi kwenye kisiwa kikuu cha Tongatapu: “Tuna safari ya saa 18 mbele yetu. Hatuwezi kusafiri bila kusimama kwa sababu ya wale ambao hupatwa na kichefuchefu. Tunafurahi sana kwenda nyumbani lakini pia tunasikitika kuwaacha watu wengi sana ambao sasa wamesikia ujumbe wa Ufalme. Tunawaacha mikononi mwa Yehova, roho yake takatifu na malaika wake wawasaidie kukua kiroho.”

  • Marafiki wa Mungu Katika Visiwa vya Tonga
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Desemba 15
    • [Picha katika ukurasa wa 10]

      Mashua “Quest” ilitumiwa kueneza habari njema huko Tonga

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki