Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ladha—Zawadi ya Muumba Mwenye Upendo
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Fungu la Ulimi

      Kiungo kikuu katika hisi yetu ya kuonja ni ulimi. Nyingi za seli onji zetu ziko katika ulimi, ijapokuwa nyingine ziko katika sehemu nyingine za kinywa na umio. Chunguza kwa umakini ulimi wako kwenye kioo. Ona michomozo mingi sana midogo ambayo hufanya ulimi wako uwe kama mahameli. Michomozo hii huitwa papillae. Seli onji ndogo-ndogo hujikusanya ndani ya papillae kwenye uso wa ulimi. “Kila seli onji ina chembe 100 au zaidi za kuonja,” lasema gazeti Science, “ambazo zinapochochewa, huamsha chembe ya neva ambayo hupeleka ujumbe kwenye ubongo.”

      Idadi ya seli onji yaweza kutofautiana sana katika watu mbalimbali na hivyo kuathiri ladha. Ulimi wa mwanadamu waweza kuwa na seli onji 10,000 au chache kama 500. Inglis Miller, aliyechunguza muundo wa seli onji alisema hivi: “Watu walio na seli onji nyingi huonja ladha nyingi; watu walio na seli onji chache huonja ladha chache.”

      Jinsi Ambavyo Kuonja Hufanya Kazi

      Hisi ya kuonja ni yenye utata sana. Kwa kweli, ni jambo la kikemia. Vipande vilivyoyeyuka vya kemikali kutoka kwenye chakula mdomoni mwetu huchochea vipokea ladha ambavyo hujitokeza kwenye vitundu vidogo katika ulimi wetu. Chembe za vipokea ladha hufanya kazi na kuchochea chembe za neva (nyuroni) kupeleka ishara kutoka kwa seli onji mpaka kwenye ubongo.

      Kwa kushangaza, seli onji moja yaweza kuchochea nyuroni nyingi tofauti-tofauti, na nyuroni moja yaweza kupokea ujumbe kutoka kwa seli onji kadhaa. Hakuna mtu ajuaye kabisa jinsi vipokezi vya ladha na mfumo wake ulio tata hufanya kazi. Kitabu The Encyclopedia Americana chasema: “Hisi zinazohisiwa katika ubongo kwa wazi hutokana na mfumo tata wa mipwito ya elektroni inayopitishwa na chembe za kupokea ladha.”

  • Ladha—Zawadi ya Muumba Mwenye Upendo
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Kwa upande mwingine, kama makala hiyo iendeleavyo kusema, “hisi ya kuonja . . . ni sahili sana. Sisi hutofautisha asili nne (na ni asili nne pekee) za kuonja: utamu, -enye chumvi, chachu, na chungu.” Ijapokuwa watu wamependa kugawanya ulimi katika sehemu za kuhisi ladha, sasa inaaminiwa kwamba seli onji moja iliyo mahali popote katika ulimi yaweza kugundua asili kadhaa au zote nne za ladha.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki