-
Nilitaka Kuwa Kama Binti ya YefthaMnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 1
-
-
“Endelea Kuboresha Ustadi Wako”
Baada ya miaka miwili na nusu hivi tukapata mgawo mpya, jijini Bombay. Elizabeth aliendelea na kazi ya kuhubiri, nami nikaombwa nimsaidie baba yangu ambaye alikuwa akitafsiri peke yake machapisho ya Biblia katika lugha ya Kannada. Alifurahia sana msaada wangu kwa sababu alikuwa na majukumu mengi kutanikoni.
Mwaka wa 1966, wazazi wangu waliamua kurudi Udipi, eneo tulilokuwa tukiishi zamani. Kabla ya kuondoka Bombay, Baba aliniambia: “Endelea kuboresha ustadi wako, binti yangu. Tafsiri kwa maneno rahisi na yanayoeleweka. Epuka kujiamini sana, na uendelee kuwa mnyenyekevu. Mtegemee Yehova.” Hayo ndiyo mashauri ya mwisho aliyonipa kwa sababu alikufa muda mfupi baada ya kurudi Udipi. Nimejitahidi kufuata mashauri yake mpaka leo ninapoendelea kufanya kazi ya kutafsiri.
-
-
Nilitaka Kuwa Kama Binti ya YefthaMnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 29]
Nikiwa na wafanyakazi wenzangu katika ofisi ya kutafsiri
-