-
Afrika Kusini2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Haikuwa rahisi kuwapelekea kweli ya Biblia watu wa jamii mbalimbali nchini Namibia. Hakukuwa na kichapo chochote cha Biblia katika lugha za kienyeji, kama vile Kiherero, Kikwangali, na Kindonga. Mwanzoni, wenyeji waliokuwa na elimu na ambao walikuwa wakijifunza Biblia, walitafsiri trakti na broshua kadhaa wakisimamiwa na Mashahidi wenyeji. Esther Bornman, aliyekuwa painia wa pekee wakati huo, alijifunza Kikwanyama na baada ya muda angeweza kukizungumza vizuri hali kadhalika lugha nyingine ya kienyeji. Yeye na Aina Nekwaya, dada anayezungumza Kindonga, walitafsiri gazeti la Mnara wa Mlinzi, ambalo huchapishwa kwa sehemu katika Kikwanyama na Kindonga. Lugha hizo mbili zinatumiwa huko Ovamboland na watu wengi wanazielewa.
Mwaka wa 1990, ofisi ya kutafsiri yenye vifaa vya kutosha ilianzishwa huko Windhoek. Watafsiri zaidi wakaongezwa, na mbali na lugha zilizotangulia kutajwa, vichapo vinatafsiriwa katika Kiherero, Kikwangali, Kikhoekhoegowab, na Kimbukushu. André Bornman na Stephen Jansen wanasimamia ofisi hiyo.
-
-
Afrika Kusini2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Ofisi ya kutafsiri ya Namibia
-