-
Shangwe ya Ushindi na HuzuniAmkeni!—1997 | Desemba 22
-
-
Kinga na Ponyo
Jambo gani linafanywa kupambana na dharura hii ya duniani pote? Njia bora zaidi ya kudhibiti ugonjwa huu ni kuugundua na kuwatibu wagonjwa wanapokuwa katika hatua za mwanzo. Hili si kwamba linawasaidia wale ambao tayari ni wagonjwa bali pia huzuia kuenea kwa ugonjwa huu kwa wengine.
Kifua kikuu kikiachwa bila kutibiwa, huua zaidi ya nusu ya wahasiriwa wake. Lakini, kitibiwapo barabara, kifua kikuu kinatibika karibu katika kila kisa ikiwa hakikusababishwa na viini vilivyo sugu kwa dawa aina kadhaa.
Kama ambavyo tumeona, matibabu yenye matokeo hutaka wagonjwa kutumia dawa hadi wamalize kiasi kihitajiwacho. Mara nyingi, hawamalizi. Kwa nini? Kukohoa, homa, na dalili nyingine kwa kawaida huisha majuma machache baada ya matibabu kuanza. Hivyo, wagonjwa wengi hufikia mkataa kwamba wamepona na kuacha kutumia dawa.
Katika kukabiliana na tatizo hili, WHO hutia moyo programu iitwayo, DOTS, ambayo ni kifupi cha “matibabu ya kuangalia wagonjwa moja kwa moja, kwa kipindi kifupi.” Kama jina hilo lidokezavyo, wafanyakazi wa afya huangalia kuhakikisha kwamba wagonjwa wao wameza dawa zote walizopangiwa, angalau kwa miezi miwili ya kwanza ya matibabu. Lakini, hili haliwi rahisi wakati wote kulifanya kwa sababu wengi wa wale walioambukizwa kifua kikuu waishi ukingoni mwa jamii. Kwa vile mara nyingi maisha yao yamejaa msukosuko na matatizo—baadhi yao hata hawana makao—ugumu wa kuhakikisha kwamba wanameza dawa zao waweza kuwa mkubwa sana.
-
-
Suluhisho la Duniani Pote—Je, Lawezekana?Amkeni!—1997 | Desemba 22
-
-
WATAALAMU wakubaliana kwamba kifua kikuu ni tatizo la duniani pote ambalo lahitaji suluhisho la duniani pote. Hakuna nchi iwezayo kudhibiti kifua kikuu ikiwa peke yake, kwani mamilioni ya watu huvuka mipaka ya kimataifa kila juma.
Wengi waamini kwamba ushirikiano wa kimataifa, huhitaji mataifa tajiri kusaidia mataifa maskini, ambayo yamekumbwa sana na kifua kikuu. Kama Dakt. Arata Kochi asemavyo, “ni kwa faida ya mataifa tajiri kusaidia mataifa yasiyoendelea ili kupambana na kifua kikuu, kabla nchi zao hazijawa uwanja wa mapambano.”
Lakini mataifa tajiri, yakiwa yanahangaishwa na mambo wayaonayo kuwa ya kutangulizwa zaidi na matatizo, hayajachukua hatua za haraka kusaidia nchi maskini kupambana na kifua kikuu. Baadhi ya nchi maskini mara nyingi huacha kukazia uangalifu utunzaji wa afya, badala ya hivyo zikitumia fedha nyingi katika zana za vita. Kufikia katikati ya mwaka 1996, ni asilimia 10 tu ya wagonjwa wa kifua kikuu ulimwenguni waliokuwa wakitibiwa kwa mbinu ya DOTS, ambao ni wachache sana kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.
Shirika la WHO laonelea hivi: “Ujuzi na dawa zisizo ghali za kutibu kifua kikuu zimekuwepo kwa miongo kadhaa. Kile ambacho ulimwengu wahitaji sasa ni juhudi zenye sulubu kutoka kwa watu wenye uwezo, uvutano na huruma ambao watahakikisha kwamba dawa hizi zinatumika kwa mafanikio ulimwenguni pote.”
-