-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na ishara kubwa ilionekana katika mbingu, mwanamke amepambwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya nyayo zake, na juu ya kichwa chake palikuwa na taji la nyota kumi na mbili,
-
-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Angalia kwamba yeye amevikwa taji la nyota 12. Nambari 12 inashirikishwa na ukamili katika mazingira ya kitengenezo.a Kwa sababu hiyo, hizi nyota 12 zinaonekana kuonyesha kwamba yeye ni mpango wa kitengenezo katika mbingu, kama vile Yerusalemu la kale lilivyokuwa duniani. Yerusalemu juu ni tengenezo la Yehova la ulimwengu wote mzima la viumbe wa roho ambalo hutenda kama mke wake, katika kumtumikia na katika kutokeza uzao.
6. (a) Ni nini kinachoonyeshwa na uhakika wa kwamba huyo mwanamke anayeonwa na Yohana amevaa joho-jua, ana mwezi chini ya nyayo zake, na ana taji la nyota? (b) Ni nini kinachofananishwa na maumivu ya kuzaa ya huyo mwanamke mwenye mimba?
6 Yohana huona mwanamke huyu akiwa amevaa joho-jua na akiwa na mwezi chini ya nyayo zake. Tunapoongeza taji la nyota, anazungukwa kabisa na nuru za kimbingu. Upendeleo wa Yehova hung’aa juu yake mchana na usiku.
-