Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Ni Nani Ambaye Anastahili Kufungua Hati-Kunjo?”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 16. (a) Katika mfumo wa mambo wa Kikristo, ni nani wanaopenya ndani ya Patakatifu Zaidi Sana palipofananishwa? (b) Ni kwa nini Wakristo wapakwa-mafuta sharti ‘wachome uvumba’?

      16 Katika mfumo wa mambo wa Kikristo, anayepata kuingia Patakatifu Zaidi Sana palipofananishwa, mahali pa kuwapo kwa Yehova katika mbingu, si Kuhani Mkuu tu aliyefananishwa, yaani, Yesu Kristo, bali hatimaye kila mmoja wa makuhani wa chini 144,000 pia hupata kupaingia. (Waebrania 10:19-23) Mwingio ndani wa hapa Patakatifu Zaidi Sana hauwezekani kwa makuhani hawa, kama wanavyowakilishwa hapa na wale wazee 24, isipokuwa wao ‘wachome uvumba,’ yaani, watoe sala na dua kwa Yehova kwa kuendelea.—Waebrania 5:7; Yuda 20, 21; linga Zaburi 141:2.

      Wimbo Mpya

      17. (a) Ni wimbo gani mpya wanaoimba wale wazee 24? (b) Usemi huo “wimbo mpya” hutumiwaje kwa kawaida katika Biblia?

      17 Sasa wimbo wa kimelodia wasikika. Anaimbiwa Mwana-Kondoo na washiriki wenzake wa kikuhani, wale wazee 24: “Na wao huimba wimbo mpya, kusema: ‘Wewe wastahili kuchukua hati-kunjo na kufungua vifungo vyayo, kwa sababu wewe ulichinjwa na kwa damu yako wewe ulinunua watu kwa ajili ya Mungu kutoka kila kabila na ulimi na kikundi cha watu na taifa.’” (Ufunuo 5:9, NW)

  • “Ni Nani Ambaye Anastahili Kufungua Hati-Kunjo?”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 18. Ni kwa ajili ya nini wazee 24 wanamsifu Yesu wakiwa na wimbo wao mpya?

      18 Ingawa hivyo, hapa, wale wazee 24 wanaimba wimbo mpya mbele ya Yesu badala ya mbele za Yehova. Lakini kanuni ni ile ile. Wao wanamsifu Yesu kwa ajili ya vitu vipya ambavyo yeye, akiwa Mwana wa Mungu, amewafanyia. Kwa njia ya damu yake, yeye alipatanisha agano jipya na hivyo akafanya kuwezekane kule kutokezwa kwa taifa jipya likiwa miliki ya pekee ya Yehova. (Warumi 2:28, 29; 1 Wakorintho 11:25; Waebrania 7:18-25) Washiriki wa hili taifa jipya la kiroho walitoka kwa mataifa mengi ya kimnofu, lakini Yesu aliwaunganisha kuwa kundi moja wawe taifa moja.—Isaya 26:2; 1 Petro 2:9, 10.

      19. (a) Ni baraka gani ambazo Israeli wa kimnofu walishindwa kupata kwa sababu ya kutoaminika kwao? (b) Taifa jipya la Yehova linapata kufurahia baraka gani?

      19 Wakati Yehova alipofanyiza Waisraeli wa kale kuwa taifa huko nyuma katika siku za Musa, yeye alifanya agano pamoja nao na akaahidi kwamba ikiwa wao wangebaki wakiwa waaminifu kwa agano hilo, wao wangekuwa ufalme wa makuhani mbele zake. (Kutoka 19:5, 6) Waisraeli hawakuwa waaminifu na kwa hiyo hawakupata kamwe utimizo wa ahadi hiyo. Kwa upande mwingine, taifa jipya, lililofanyizwa kwa thamani ya agano jipya lenye kupatanishwa na Yesu, limebaki likiwa jaminifu. Basi washiriki walo wanapata kutawala juu ya dunia wakiwa wafalme na pia wanatumikia wakiwa makuhani, wakisaidia wale wenye mioyo inayofaa miongoni mwa aina ya binadamu wapatanishwe kwa Yehova. (Wakolosai 1:20) Ni kama vile ule wimbo mpya unavyoonyesha hilo: “Na wewe ulifanya wao kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu, nao wanapaswa kutawala wakiwa wafalme juu ya dunia.” (Ufunuo 5:10, NW)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki