-
“Ni Nani Ambaye Anastahili Kufungua Hati-Kunjo?”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na wakati alipotwaa ile hati-kunjo, wale viumbe hai wanne na wale wazee ishirini na wanne walianguka chini mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja akiwa na kinubi na mabakuli ya dhahabu yaliyokuwa yamejaa uvumba, na huo uvumba humaanisha sala za watakatifu.” (Ufunuo 5:8, NW) Kama wale viumbe hai wanne wa kikerubi mbele ya kiti cha ufalme cha Mungu, wazee 24 wanainamia Yesu katika kukiri mamlaka yake. Lakini hao wazee wako peke yao katika kuwa na vinubi na mabakuli ya uvumba.a Na wao peke yao sasa waimba wimbo mpya. (Ufunuo 5:9) Hivyo wanafanana na wale 144,000 wa “Israeli wa Mungu” watakatifu, ambao pia wanabeba vinubi na kuimba wimbo mpya. (Wagalatia 6:16; Wakolosai 1:12; Ufunuo 7:3-8; 14:1-4) Na zaidi, wale wazee 24 wanaonyeshwa wakitimiza utendaji wa kikuhani wa kimbingu, uliofananishwa na ule wa makuhani katika Israeli wa kale ambao walimchomea Yehova uvumba katika ile tabenakulo—utendaji ambao ulikwisha wakati Yehova alipoioondolea mbali ile Sheria ya Musa, akiigongomelea penye nguzo ya mateso ya Yesu. (Wakolosai 2:14) Tunakata neno gani kutokana na haya yote? Kwamba hapa wale washindi wapakwa-mafuta wanaonekana wakiwa katika mgawo wao wa mwisho kabisa wakiwa ‘makuhani wa Mungu na wa Kristo, wakitawala wakiwa wafalme pamoja naye kwa miaka elfu.’—Ufunuo 20:6, NW.
-
-
“Ni Nani Ambaye Anastahili Kufungua Hati-Kunjo?”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
16. (a) Katika mfumo wa mambo wa Kikristo, ni nani wanaopenya ndani ya Patakatifu Zaidi Sana palipofananishwa? (b) Ni kwa nini Wakristo wapakwa-mafuta sharti ‘wachome uvumba’?
16 Katika mfumo wa mambo wa Kikristo, anayepata kuingia Patakatifu Zaidi Sana palipofananishwa, mahali pa kuwapo kwa Yehova katika mbingu, si Kuhani Mkuu tu aliyefananishwa, yaani, Yesu Kristo, bali hatimaye kila mmoja wa makuhani wa chini 144,000 pia hupata kupaingia. (Waebrania 10:19-23) Mwingio ndani wa hapa Patakatifu Zaidi Sana hauwezekani kwa makuhani hawa, kama wanavyowakilishwa hapa na wale wazee 24, isipokuwa wao ‘wachome uvumba,’ yaani, watoe sala na dua kwa Yehova kwa kuendelea.—Waebrania 5:7; Yuda 20, 21; linga Zaburi 141:2.
-
-
“Ni Nani Ambaye Anastahili Kufungua Hati-Kunjo?”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Picha ya ukurasa mzima katika ukurasa wa 86]
-