-
Yehova Aharibu Kiburi cha TiroUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
21. Tiro ‘limesahauliwaje,’ na kwa muda gani?
21 Isaya aendelea kutoa unabii: “Itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja.” (Isaya 23:15a) Baada ya Wababiloni kuliharibu jiji la barani, jiji la kisiwani la Tiro ‘litasahauliwa.’ Sawasawa kabisa na unabii huo, kwa muda wa “mfalme mmoja”—Milki ya Babiloni—jiji la kisiwani la Tiro halitakuwa kitovu muhimu kiuchumi. Yehova, kupitia Yeremia, aweka Tiro kati ya mataifa yatakayotengwa ili yanywe divai ya hasira Yake kali. Asema: “Mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.” (Yeremia 25:8-17, 22, 27) Ni kweli kwamba jiji la kisiwani la Tiro haliwi chini ya Babiloni kwa miaka 70 kamili, kwa vile Milki ya Babiloni yaanguka mwaka wa 539 K.W.K. Yaonekana kwamba miaka 70 huwakilisha kipindi cha utawala mkuu wa Babiloni ambapo nasaba ya wafalme ya Babiloni yajisifu kuwa imeinua kiti chake cha ufalme hata juu ya “nyota za Mungu.” (Isaya 14:13) Mataifa mbalimbali yaja chini ya utawala huo nyakati mbalimbali. Lakini mwishoni mwa miaka 70, utawala huo utaanguka. Ni nini kitakacholipata Tiro wakati huo?
22, 23. Ni nini kitakachotendeka kwa Tiro litokapo chini ya utawala wa Babiloni?
22 Isaya aendelea: “Hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba.
-
-
Yehova Aharibu Kiburi cha TiroUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
23 Baada ya kuanguka kwa Babiloni mwaka wa 539 K.W.K., Foinike yawa koloni la Milki ya Umedi na Uajemi. Mtawala Mwajemi, Koreshi Mkuu, ni mtawala anayetoa uhuru zaidi. Chini ya utawala wake mpya, Tiro litaanza tena utendaji wake wa awali na kujitahidi sana kupata umaarufu wake wa kuwa kituo cha kibiashara—kama vile kahaba ambaye amesahauliwa na kupoteza wateja wake atafutavyo kuvutia wateja wapya kwa kutembea jijini, akipiga kinubi chake na kuimba nyimbo zake.
-