Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Sheria ya Bwana Ni Kamilifu”
    Mkaribie Yehova
    • 9, 10. Agano la Sheria lilisema nini kuhusu ngono na kujifungua mtoto, na sheria hizo zilikuwa na manufaa gani?

      9 Agano la Sheria lilisema kwamba mtu aliyejifungua mtoto au kufanya ngono—hata kati ya wenzi wa ndoa—angekuwa najisi kwa kipindi fulani. (Mambo ya Walawi 12:2-4; 15:16-18) Sheria hizo hazikudharau zawadi hizo safi kutoka kwa Mungu. (Mwanzo 1:28; 2:18-25) Badala yake, sheria hizo zilidumisha utakatifu wa Yehova kwa kuwazuia waabudu wake wasichafuliwe. Kumbuka kwamba mataifa jirani ya Israeli yalikuwa yakichanganya dini na ibada za ngono na uzazi. Dini ya Wakanaani ilikuwa na makahaba wa kiume na wa kike. Walitenda mambo maovu kupindukia na yakaenea kotekote. Kinyume chake, Sheria ilitenga kabisa ibada ya Yehova na mambo ya ngono.b Kulikuwa na faida nyingine pia.

      10 Sheria hizo pia zilifundisha ukweli fulani muhimu sana.c Dhambi ya Adamu inapitishwaje kutoka kizazi hadi kizazi? Ni kupitia ngono na kuzaa, sivyo? (Waroma 5:12) Ndiyo, Sheria ya Mungu iliwakumbusha watu wake kwamba wao ni watenda-dhambi. Kwa kweli, sote tunazaliwa katika dhambi. (Zaburi 51:5) Tunahitaji msamaha na ukombozi ili kumkaribia Mungu wetu mtakatifu.

  • “Sheria ya Bwana Ni Kamilifu”
    Mkaribie Yehova
    • b Mahekalu ya Wakanaani yalikuwa na vyumba vya kufanyia ngono, lakini Sheria ya Musa ilisema kwamba watu wote walio najisi hawangeweza hata kuingia hekaluni. Kwa hiyo, hakuna mtu yeyote angechanganya ngono na ibada katika nyumba ya Yehova, kwa sababu ngono ilimfanya mtu awe najisi kwa kipindi fulani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki