Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Fumbo Lenye Kutia Hofu Lafumbuliwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Amani na Usalama —Tumaini la Bure

      10, 11. (a) UM ulipiga mbiu ya nini katika 1986, na itikio lilikuwa nini? (b) Ni “jamaa za kidini” ngapi zilizokusanyika katika Assisi, Italia, kusali kwa ajili ya amani, na je! Mungu anajibu sala kama hizo? Fafanua.

      10 Katika jitihada za kutegemeza matumaini ya aina ya binadamu, Umoja wa Mataifa ulipiga mbiu ya 1986 kuwa “Mwaka wa Amani ya Kimataifa,” ukiwa na kichwa “Kulinda Salama Amani na Wakati Ujao wa Binadamu.” Mataifa yenye kupiga vita yaliombwa yalaze silaha zayo, angalau kwa mwaka mmoja. Itikio layo lilikuwa nini? Kulingana na ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa, watu wapatao milioni tano walikufa kwa sababu ya vita wakati wa 1986 pekee! Ingawa sarafu kadhaa za pekee na stampu za mwadhimisho zilitolewa, mataifa yaliyo mengi yalifanya kidogo sana kwa habari ya kufuatia wazo bora la amani katika mwaka huo.

  • Fumbo Lenye Kutia Hofu Lafumbuliwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 250]

      Kinyume cha “Amani”

      Ingawa 1986 ulipigiwa mbiu na UM kuwa Mwaka wa Amani ya Kimataifa, shindano la ujiuaji la kuunda silaha liliongezeka. World Military and Social Expenditures 1986 hutoa fasili hizi zenye kumakinisha:

      Katika 1986 matumizi ya kijeshi ya tufe lote yalifikia dola milioni elfu 900.

      Matumizi ya kijeshi ya tufe lote ya saa moja yangetosha kuchanja watu milioni 3.5 ambao walikufa kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuambukiza yenye kuzuilika.

      Ulimwenguni pote, mtu mmoja kati ya watano aliishi katika umaskini wenye kuumiza. Watu hao wote wenye kufa-njaa wangeweza kulishwa kwa mwaka mmoja kwa gharama ya kile kiasi ambacho ulimwengu ulitumia kwa ajili ya silaha katika siku mbili.

      Nishati ya baruti iliyo katika rundo la silaha za nyukilia za ulimwengu ilikuwa kubwa zaidi ya ule mlipuko wa Chernobyl kwa mara 160,000,000.

      Bomu moja la nyukilia lingeweza kupelekwa likiwa na nguvu za mlipuko mara zaidi ya 500 ya bomu lililoangushwa juu ya Hiroshima katika 1945.

      Maghala ya zana za nyukilia yalikuwa na nguvu za baruti zinazolingana na Hiroshima zaidi ya milioni moja. Yaliwakilisha mara 2,700 za nguvu za baruti zilizoachiliwa katika Vita ya Ulimwengu 2, wakati watu milioni 38 walikufa.

      Vita vilikuwa vikitokea mara nyingi zaidi na ni vyenye kufisha zaidi. Vifo kutokana na vita vilikuwa jumla ya milioni 4.4 katika karne ya 18, milioni 8.3 katika karne ya 19, milioni 98.8 katika miaka 86 ya kwanza ya karne ya 20. Tangu karne ya 18, vifo kutokana na vita vimeongezeka zaidi ya mara sita kuliko idadi ya watu ya ulimwengu. Kulikuwako vifo mara kumi kwa kila vita katika karne ya 20 kuliko ilivyokuwa katika karne ya 19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki