-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na yeye [malaika] akapeleka mimi mbali kwa nguvu ya roho kuingia ndani ya jangwa. Na mimi nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ambaye alikuwa amejaa majina ya kufuru na ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”—Ufunuo 17:3, NW.
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
16. Ni nini utambulisho wa huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na imetaarifiwa nini kwa habari ya kusudi lake?
16 Basi, hayawani-mwitu mpya rangi-nyekundu-nyangavu ni nini? Yeye ni lazima awe ule mfano wa hayawani-mwitu ambao ulitokezwa kwa himizo la hayawani-mwitu Uingereza-Amerika aliyekuwa na pembe mbili mithili ya mwana-kondoo. Baada ya mfano huo kuwa umefanywa, huyo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili aliruhusiwa kuupa pumzi huo mfano wa hayawani-mwitu. (Ufunuo 13:14, 15) Yohana anaona sasa mfano ulio hai, unaopumua. Ni picha ya tengenezo la Ushirika wa Mataifa ambalo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alileta kwenye uhai katika 1920. Rais Wilson wa U.S. alikuwa na njozi ya kwamba Ushirika huo “ungekuwa baraza la kutolea watu wote haki na kufutilia mbali milele tisho la vita.” Lilipofufuliwa baada ya vita ya ulimwengu ya pili likiwa Umoja wa Mataifa, kusudi la katiba yalo lilikuwa “kudumisha amani na usalama wa kimataifa.”
-