-
Washiriki Wapya wa Baraza LinaloongozaMnara wa Mlinzi—2000 | Januari 1
-
-
Washiriki Wapya wa Baraza Linaloongoza
MNAMO Jumamosi, Oktoba 2, 1999, Mkutano wa Kila Mwaka wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania ulimalizika kwa tangazo ambalo halikutarajiwa. Watu 10,594 waliohudhuria au waliosikiliza kupitia simu walisisimka kusikia kwamba washiriki wapya wanne walikuwa wameongezwa kwenye Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova. Washiriki hao wapya, wote Wakristo watiwa-mafuta, ni Samuel F. Herd; M. Stephen Lett; Guy H. Pierce; na David H. Splane.
-
-
Washiriki Wapya wa Baraza LinaloongozaMnara wa Mlinzi—2000 | Januari 1
-
-
• David Splane alianza upainia Septemba 1963. Alihitimu darasa la 42 la Gileadi, akatumikia akiwa mishonari nchini Senegal, Afrika, kisha akawa mwangalizi wa mzunguko nchini Kanada kwa miaka 19. Yeye pamoja na mke wake, Linda, wamekuwa washiriki wa Betheli ya Marekani tangu mwaka wa 1990, ambako Ndugu Splane ametumikia katika idara ya Utumishi na ya Uandikaji. Tangu mwaka wa 1998, amekuwa msaidizi wa Halmashauri ya Uandikaji.
-