Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi Uliopo
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • b Mnamo 1995, wanasayansi waliona tabia ya ajabu ya nyota (SN 1995K), iliyo ya mbali zaidi iliyopata kuonekana ikilipuka katika kundi lake. Kama ilivyo na milipuko mikubwa sana ya nyota katika makundi yaliyo karibu, nyota hiyo ikawa nyangavu sana kisha ikafifia polepole ikichukua muda mrefu kuliko ilivyopata kuonekana awali. Gazeti New Scientist lilichora grafu na kueleza hivi: “Nuru kutoka kwenye nyota iliyokuwa ikilipuka mbali . . . ilionekana ikichukua muda mrefu uliotarajiwa iwapo kundi hilo la nyota lilikuwa likienda mbali na dunia kwa karibu nusu ya mwendo wa nuru.” Gazeti hilo lafikia uamuzi gani? Huu ni “uthibitisho bora zaidi wa kwamba kwa kweli Ulimwengu unapanuka.”

  • Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi Uliopo
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • Uthibitisho Unaoonyesha Kulikuwa na Mwanzo

      Nyota zote unazoweza kuona ziko katika Kilimia. Kufikia miaka ya 1920, watu walidhani kwamba hakukuwa na kundi jingine la nyota ila hilo tu. Ingawa hivyo, labda unajua kwamba uchunguzi uliofanywa na darubini kubwa umethibitisha kwamba hiyo si kweli. Ulimwengu wetu una angalau makundi 50,000,000,000 ya nyota. Hatumaanishi nyota bilioni 50—lakini angalau makundi bilioni 50 ya nyota, na kila kundi lina mabilioni ya nyota zinazofanana na jua letu. Lakini, si wingi huo wa makundi makubwa-makubwa ya nyota uliowashtua wanasayansi katika miaka ya 1920. Jambo lililowashtua ni kwamba makundi hayo yote yako mwendoni.

      Wataalamu wa nyota waligundua jambo moja lenye kutokeza sana: Nuru inayotoka kwenye kundi la nyota ilipopitishwa kwenye kipande cha glasi kinachotawanya nuru, mawimbi ya nuru yalionekana yakiwa yamerefuka, ikionyesha kwamba makundi ya nyota yaliyo mbali na dunia yalikuwa katika mwendo wa kasi sana. Kadiri kundi la nyota lilivyokuwa mbali zaidi, ndivyo lilivyoonekana kwenda kasi sana mbali na dunia. Hilo ladokeza kwamba ulimwengu unapanuka!b

      Hata kama sisi si wataalamu wa nyota wala wapenzi wa mambo ya nyota, twaweza kuona kwamba upanuzi wa ulimwengu unaweza kuashiria mambo mengi sana kuhusu wakati wetu uliopita—na labda wakati wetu ujao vilevile. Ni lazima kitu fulani kilianzisha upanuzi wa ulimwengu—kitu chenye uwezo sana kuliko nguvu nyingi za uvutano za ulimwengu. Mtu anakuwa na sababu nzuri ya kuuliza, ‘Ni nini kingeweza kusababisha nguvu nyingi sana hivyo?’

      Ingawa wanasayansi wengi husema ulimwengu ulianza ukiwa kitu kidogo sana ambacho kilifinyana sana, hatuwezi kuepuka suala hili kuu: “Ikiwa wakati fulani uliopita, Ulimwengu ulikuwa kitu kidogo sana kisichoweza kuwazika na chenye uzito usioweza kuwazika, ni lazima tuulize ni nini kilichokuwapo hapo awali na nini kilichokuwapo nje ya Ulimwengu. . . . Ni lazima tukabili suala la kuwapo kwa Chanzo fulani.”—Sir Bernard Lovell.

      Hili ladokeza zaidi ya kuwapo tu kwa chanzo cha nishati nyingi. Busara na akili pia zinahitajiwa kwa sababu kiwango cha upanuzi wa ulimwengu chaonekana kuwa kimepimwa barabara kabisa. “Ikiwa kiwango cha upanuzi wa Ulimwengu kingeongezeka hata kwa kiasi cha sehemu moja tu ya milioni moja mara milioni moja,” asema Lovell, “basi kufikia sasa kila kitu kilichomo Ulimwenguni kingekuwa kimetawanyika. . . . Na ikiwa kiwango hicho kingalipungua hata kwa kiasi cha sehemu moja tu ya milioni moja mara milioni moja, basi nguvu za uvutano zingalisababisha Ulimwengu uporomoke miaka ipatayo milioni elfu moja ya kwanza. Hapa tena twaona ya kwamba hakungekuwa na nyota zenye kudumu na basi hakungekuwa na uhai.”

  • Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi Uliopo
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • [Picha katika ukurasa wa 14]

      Mtaalamu wa nyota Edwin Hubble (1889-1953) alitambua kwamba badiliko jekundu katika nuru kutoka kwenye makundi ya mbali ya nyota lilionyesha kwamba ulimwengu wetu unapanuka na kuthibitisha kwamba ulikuwa na mwanzo

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki