-
‘Nafsi Zilizochinjwa’ ZathawabishwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
5. Ni kwa jinsi gani nafsi za waaminifu, zijapokuwa zimekufa, zinalia kwa sauti kubwa ili kisasi kilipwe?
5 Ule mfululizo wa mandhari waendelea kufunguka: “Na hizo zikalia kwa sauti kubwa, zikisema: ‘Ni mpaka lini, Bwana Mwenye Enzi Kuu mtakatifu na wa kweli, wewe unajizuia usihukumu na kulipiza kisasi damu yetu juu ya wale ambao wanakaa juu ya dunia?’” (Ufunuo 6:10, NW) Nafsi zao, au damu, zingeweza kuliaje kwa kutaka kisasi, kwa kuwa Biblia inaonyesha kwamba wafu hawana fahamu? (Mhubiri 9:5) Basi, je! damu ya Abeli mwadilifu haikulia kwa sauti kubwa wakati Kaini alipomwua kimakusudi? Ndipo Yehova alipomwambia Kaini hivi: “Wewe umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kwa sauti kubwa kutoka ardhi.” (Mwanzo 4:10, 11, NW; Waebrania 12:24) Si kwamba damu ya Abeli ilikuwa ikitamka maneno kihalisi. Badala ya hivyo, Abeli alikuwa amekufa akiwa jeruhi asiye na hatia, nayo haki ililia kwa sauti kubwa ikitaka mwuaji kimakusudi wake aadhibiwe. Hali moja na hiyo, Wakristo hao wafia-imani hawana hatia, na kwa haki lazima walipiwe kisasi. (Luka 18:7, 8) Kilio cha kutaka kisasi kilipwe ni kikuu kwa sababu maelfu wengi wamekufa.—Linga Yeremia 15:15, 16.
6. Ni umwagaji-damu gani usio na hatia uliolipizwa kisasi katika 607 K.W.K.?
6 Hali hiyo ingeweza kufananishwa pia na ile iliyokuwa Yuda yenye kuasi imani wakati Mfalme Manase alipokuja kukalia kiti cha ufalme katika 716 K.W.K. Yeye alimwaga damu nyingi isiyo na hatia, pengine ‘akimpasua vipande vipande kwa msumeno’ nabii Isaya. (Waebrania 11:37, NW; 2 Wafalme 21:16) Ijapokuwa baadaye Manase alitubu na akabadilika, hiyo hatia ya damu ilibaki. Katika 607 K.W.K., wakati Wababuloni walipouacha ukiwa ufalme wa Yuda, “ilikuwa tu kwa amri ya Yehova kwamba hilo likatukia dhidi ya Yuda, kuiondoa machoni pake kwa ajili ya madhambi ya Manase, kulingana na yale yote ambayo yeye alikuwa amefanya; na pia kwa ajili ya damu isiyo na hatia ambayo yeye alikuwa amemwaga, hivi kwamba yeye alijaza Yerusalemu damu isiyo na hatia, na Yehova hakuidhini kutoa msamaha.”—2 Wafalme 24:3, 4, NW.
7. Ni nani hasa mwenye hatia ya ‘umwagaji-damu ya watakatifu’?
7 Kama vile katika nyakati za Biblia, ndivyo na leo, wengi wa wale watu mmoja mmoja walioua mashahidi wa Mungu huenda wamekufa kitambo. Lakini tengenezo lililosababisha ufia-imani wao lingali hai sana na ni lenye hatia ya damu. Ni tengenezo la Shetani la kidunia, mbegu yake ya kidunia. Sehemu yenye kutokeza katika hiyo ni Babuloni Mkubwa, ile milki ya ulimwengu ya dini bandia.a Yeye anaelezwa kuwa ‘amelewa kwa damu ya watakatifu na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.’ Ndiyo, “katika yeye ilipatikana damu ya manabii na ya watakatifu na ya wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” (Ufunuo 17:5, 6; 18:24; Waefeso 4:11; 1 Wakorintho 12:28, NW) Ni mzigo wa hatia ya damu kama nini! Maadamu Babuloni Mkubwa yupo, damu ya majeruhi wake italia kwa sauti kubwa kwa kutaka haki itekelezwe.—Ufunuo 19:1, 2.
8. (a) Ni mifano gani ya ufia-imani iliyokuwa imetukia wakati wa maisha ya Yohana? (b) Ni minyanyaso gani iliyochochewa na wamaliki Waroma?
8 Yohana mwenyewe alishuhudia ufia-imani katika karne ya kwanza wakati Nyoka mkatili na mbegu yake ya kidunia walipopiga vita juu ya kundi la Wakristo wapakwa-mafuta lililokuwa likikua. Yohana alikuwa ameona Bwana yetu akitundikwa juu ya nguzo na alikuwa ameishi kupitia vipindi vya kuuawa kwa Stefano, kwa ndugu yake mwenyewe Yakobo, na kwa Petro, kwa Paulo, na washiriki wengine wa karibu. (Yohana 19:26, 27; 21:15, 18, 19; Matendo 7:59, 60; 8:2; 12:2; 2 Timotheo 1:1; 4:6, 7) Katika 64 W.K., Nero, maliki Mroma alikuwa amelaumu bure Wakristo, akiwashtakia kuteketeza jiji, ili kukanusha uvumi wa kwamba ndiye aliyekuwa mwenye hatia. Mwanahistoria Takito anaripoti hivi: “Wao [Wakristo] walikufa kwa njia za dhihaka; baadhi yao walifunikwa ngozi za hayawani-mwitu kisha wakararuliwa na mbwa, baadhi yao [walitundikwa juu ya nguzo],b baadhi yao walichomwa kuwa mienge ya kunurisha usiku.” Wimbi zaidi la mnyanyaso chini ya Maliki Domitiano (81-96 W.K.) lilikuwa limetokeza kuhamishwa kwa Yohana kupelekwa kisiwa cha Patmosi. Kama Yesu alivyosema: “Ikiwa wao wamenyanyasa mimi, wao watanyanyasa nyinyi pia.”—Yohana 15:20; Mathayo 10:22, NW.
9. (a) Ni kipeo gani cha udanganyifu alichotokeza Shetani kufikia karne ya nne W.K., nacho ni sehemu kuu ya nini? (b) Baadhi ya watawala wa Jumuiya ya Wakristo waliwatendeaje Mashahidi wa Yehova wakati wa Vita ya Ulimwengu 1 na 2?
9 Kufikia karne ya nne W.K., yule nyoka wa zamani, Shetani Ibilisi, alikuwa ametokeza kipeo cha udanganyifu wake, ile dini yenye uasi-imani ya Jumuiya ya Wakristo—mfumo wa Kibabuloni uliofichwa chini ya kibandiko cha “Ukristo.” Ndiyo sehemu iliyo kuu ya mbegu ya yule Nyoka na imesitawi ikawa umati wa farakano zenye kuhitilafiana. Kama Yuda ya kale isiyo na imani, Jumuiya ya Wakristo inabeba hatia nzito ya damu, ikiwa imekwisha kujihusisha sana katika pande zote mbili za Vita ya Ulimwengu 1 na 2. Wengine wa watawala wa kisiasa wa Jumuiya ya Wakristo hata walitumia vita hivyo kuwa kisababu cha kuchinja watumishi wa Mungu. Likiripoti juu ya Hitla kunyanyasa Mashahidi wa Yehova, pitio la kitabu Kirchenkampf in Deutschland (Vita ya Makanisa Katika Ujeremani) lilitaarifu hivi: “Theluthi moja yao [Mashahidi] waliuawa, ama walifishwa kwa amri ya kiserikali, ama kwa matendo mengine ya jeuri, njaa, ugonjwa au kazi ngumu ya utumwa. Ukali wa utiisho huu ulikuwa bila kitangulizi na ulikuwa tokeo la imani thabiti ambayo haingeweza kupatanishwa na siasa ya Usoshalisti wa Kitaifa.” Kweli kweli, inaweza kusemwa juu ya Jumuiya ya Wakristo, kutia na upadri wayo: “Katika marinda yako zimepatikana alama za damu ya nafsi za maskini wasio na hatia.”—Yeremia 2:34, NW.c
10. Wanaume vijana wa ule umati mkubwa wamepatwa na minyanyaso gani katika mabara mengi?
10 Tangu 1935 wanaume vijana waaminifu wa ule umati mkubwa wamehimili ukali wa minyanyaso katika mabara mengi. (Ufunuo 7:9) Hata wakati Vita ya Ulimwengu 2 ilipokuwa ikiisha katika Ulaya, katika mji mmoja tu vijana Mashahidi wa Yehova 14 walifishwa kwa kunyongwa kwa amri ya kiserikali. Uhalifu wao? Kukataa ‘kujifunza vita tena.’ (Isaya 2:4) Karibuni zaidi, wanaume vijana katika Mashariki na katika Afrika wamepigwa mpaka kifo au wakauawa na kikosi cha wapiga risasi kwa amri ya kiserikali juu ya suala ilo hilo. Wafia-imani hawa vijana, wategemezaji wastahilifu wa ndugu za Yesu wapakwa-mafuta, hakika watapata ufufuo kuingia ndani ya ile dunia mpya iliyoahidiwa.—2 Petro 3:13; Linga Zaburi 110:3; Mathayo 25:34-40; Luka 20:37, 38.
-
-
‘Nafsi Zilizochinjwa’ ZathawabishwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Hata hivyo, mwishowe, damu yote yenye uadilifu iliyomwagwa na Babuloni Mkubwa na hawara zake wa kisiasa italipiwa kisasi. Kwa wakati uliopo, pasipo shaka wale waliofufuliwa wana shughuli wakiwa na wajibu mwingi wa kimbingu. Wao wanapumzika, si kwa kustarehe katika raha ya kutotenda, bali katika njia ya kwamba wao wanangojea kwa subira siku ya kisasi cha Yehova. (Isaya 34:8; Warumi 12:19) Pumziko lao litakwisha wakati wao watashuhudia uharibifu wa dini bandia na, wakiwa ‘walioitwa na waliochaguliwa na waaminifu,’ wao wanaandamana na Bwana Yesu Kristo katika kutekeleza hukumu hapa duniani juu ya sehemu nyingine zote za mbegu mbovu ya Shetani.—Ufunuo 2:26, 27; 17:14; Warumi 16:20.
-