Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuishi na Kuhubiri Karibu na Volkeno
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 15
    • Kuishi na Kuhubiri Karibu na Volkeno

      “NI JAMBO lenye kuogofya sana. Laweza kuwa tu kama mwisho wa ulimwengu ambao Biblia husema juu yake. Lazima tuendelee kuwa chonjo na kuwa na msimamo mzuri mbele za Yehova Mungu kila wakati.” Hayo ni maneno ya Víctor, mmoja wa Mashahidi wa Yehova, akisimulia jambo aliloona la kuishi karibu sana na volkeno ya Popocatépetl, inayojulikana sana kuwa Popo, katika Mexico.

      Volkeno hii yenye kunguruma imekuwa katika habari za kimataifa tangu 1994.a Wenye mamlaka walikata kauli kwamba kila kitu kilichoko kilometa 30 kuzunguka eneo la kreta kiko katika eneo lenye hatari kubwa sana. Upande wa kusini wa volkeno hasa ni wenye hatari kwa sababu kreta imeinama kuelekea upande huo na kuna mabonde kadhaa yenye kina kirefu ambayo kupitia hayo lava na matope yaweza kutapanywa nje ya kreta.

      Kiasili, wengi hujiuliza kile ambacho kingeweza kuipata Mexico City endapo mlipuko mkubwa wa volkeno hiyo ungetokea. Je, jiji hilo limo hatarini? Kisha pia kuna wale watu wote walio katika jimbo la Morelos kuelekea kusini mwa volkeno hiyo. Je, wote walio katika eneo hilo pia wamo hatarini? Na kuishi karibu na volkeno hiyo kukoje, bila kujua ni nini kiwezacho kutukia siku yoyote?

      Tisho la Volkeno

      Kitovu cha Mexico City kiko karibu kilometa 70 kaskazini-magharibi mwa Popocatépetl, ijapokuwa baadhi ya vitongoji viko umbali wa kilometa 40 tu. Kihalisi, eneo lote la mji mkuu, lenye idadi ya watu milioni 20, liko nje ya eneo la hatari. Hata hivyo, ikitegemea unakoelekea upepo, eneo hili laweza kuathiriwa, jivu jingi mno likitolewa na volkeno hiyo.

      Matokeo ya jivu la volkeno kwa ukawaida ni mabaya zaidi upande wa mashariki wa volkeno hiyo. Eneo hili latia ndani jiji la Puebla na idadi ya majiji na miji midogo-midogo, iliyo na watu wapatao 200,000 wanaoishi katika eneo lenye hatari kubwa sana. Jumapili, Mei 11, 1997, volkeno hiyo ilirusha tani nyingi za jivu hewani na kulieneza kote katika eneo hili, likifika hadi kwenye jimbo la Veracruz, zaidi ya kilometa 300 upande wa mashariki. Katika eneo lililo kusini mwa volkeno hiyo, katika jimbo la Morelos, kuna majiji na miji kadhaa iliyo na idadi ya watu wapatao 40,000 ambao pia wangeweza kuwa katika hatari kubwa.

  • Kuishi na Kuhubiri Karibu na Volkeno
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 15
    • Waweza Kujitayarishaje?

      Wastadi wa volkeno hufanya uchunguzi wao na kutoa ripoti rasmi kuhusu Popocatépetl itishayo, lakini kwa kweli hakuna ajuaye ni nini kitakachotukia au ni wakati gani. Kulingana na vyombo vya habari na watu wanaoishi karibu na hapo, volkeno yaweza kulipuka wakati wowote. Tisho hilo ni la kweli. Bila shaka, wenye mamlaka wanahangaika sana nao wanataka kufanya yote wawezayo kuwa tayari endapo dharura itatokea. Lakini yaeleweka kwamba lazima wawe waangalifu kuhusu kutoa onyo, kwa kuwa hawataki kuanzisha kuhama kwa watu wengi ikiwa hakuna hatari inayokaribia. Basi, mtu afanyeje?

      “Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; bali wajinga huendelea mbele wakaumia,” yasema mithali ya Biblia. (Mithali 22:3) Kwa hiyo, jambo la hekima ni kuchukua hatua zinazohitajiwa ili kuhakikisha usalama wa mtu binafsi wakati fursa ingalipo, si ‘kuendelea mbele’ kana kwamba hakuna chochote kitakachotukia, wala kungojea mlipuko kimakusudi kabla ya kuchukua hatua kana kwamba unataka kuona litakalotukia. Hivi ndivyo Mashahidi wa Yehova katika eneo hilo wanavyoona jambo hilo.

      Hivi majuzi, wawakilishi kutoka ofisi ya tawi ya Watch Tower Society walikutana na waangalizi wasafirio katika jimbo la Puebla, ambao huwasiliana sana na makutaniko yaliyo katika eneo lenye hatari. Mipango ilifanywa ili waangalizi wasafirio na washiriki wa halmashauri ya kutoa msaada watembelee kila moja ya familia zinazoishi umbali wa kilometa 25 kutoka kwenye kreta. Familia hizo zilisaidiwa kufikiria kwa uangalifu kuhama eneo lenye hatari kabla ya mlipuko. Usafiri na mahali pa kuishi palipangwa ili kupatia nafasi watu 1,500 katika jiji la Puebla. Familia nyingine zilihama zikaishi na watu wa jamaa katika majiji mengine.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki