-
Jinsi Hana Alivyopata AmaniMnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
-
-
Hana Anaweka Nadhiri
Dhabihu za ushirika zililiwa katika patakatifu pa Yehova. Baada ya kuondoka katika chumba cha kulia chakula, Hana anasali kwa Mungu. (1 Samweli 1:9, 10) “Ee Yehova wa majeshi,” Hana anasihi, “ikiwa hakika utayaona mateso ya kijakazi wako, nawe kwa kweli unikumbuke, na ikiwa hutamsahau kijakazi wako na kwa kweli umpe kijakazi wako uzao wa kiume, mimi nitamtoa kwa Yehova siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita juu ya kichwa chake.”—1 Samweli 1:11.
Hana anataja mambo hususa katika sala. Anaomba mtoto wa kiume na kuweka nadhiri kwamba mtoto huyo atawekwa wakfu kwa Yehova na kuwa Mnadhiri maisha yake yote. (Hesabu 6:1-5) Nadhiri kama hiyo inategemea kibali cha mume wake, na mambo ambayo Elkana anafanya baadaye yanaonyesha kwamba anakubali ahadi ya mke wake mpendwa.—Hesabu 30:6-8.
-
-
Jinsi Hana Alivyopata AmaniMnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
-
-
Hapana shaka kwamba tangu Samweli akiwa mtoto mchanga, Hana anaanza kumfundisha kumhusu Yehova. Lakini je, anasahau nadhiri aliyoweka? Bila shaka hapana! “Mara mvulana huyu atakapoachishwa kunyonya, nitampeleka, naye ataonekana mbele za Yehova na kukaa huko mpaka wakati usio na kipimo,” anasema. Samweli anapoachishwa kunyonya, labda akiwa na miaka mitatu au zaidi, Hana anampeleka ili aishi katika patakatifu pa Yehova, kama tu alivyoahidi katika nadhiri.—1 Samweli 1:21-24; 2 Mambo ya Nyakati 31:16.
Baada ya dhabihu kutolewa kwa Yehova, Hana na mume wake wanampeleka Samweli kwa Eli. Inaelekea sana kwamba Hana anamshika mkono mvulana huyo mdogo huku akimwambia Eli hivi: “Nakuomba radhi, bwana wangu! Kama inavyoishi nafsi yako, bwana wangu, mimi ndiye yule mwanamke aliyekuwa amesimama pamoja nawe mahali hapa ili kusali kwa Yehova. Ilikuwa kuhusu mvulana huyu kwamba nilisali ili Yehova anipe ombi langu nililomwomba. Na mimi nimemwazima Yehova mvulana huyu. Siku zote atakazokuwapo, yeye ni mtu aliyeombwa kwa ajili ya Yehova.” Hivyo ndivyo maisha ya Samweli ya utumishi wa pekee kwa Mungu yanavyoanza.—1 Samweli 1:25-28; 2:11.
-