Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 13. Ni katika njia gani watawala wa ulimwengu huu walio ufananisho wa jua ‘wameunguza’ aina ya binadamu?

      13 Baada ya vita ya ulimwengu ya kwanza, watawala wa ulimwengu huu walifanyiza Ushirika wa Mataifa katika jitihada ya kutatua tatizo la ulimwengu la usalama, lakini huu ulishindwa. Kwa hiyo aina nyingine za utawala wa kujaribia zilionjwa, kama vile Ufashisti na Unazi. Ukomunisti uliendelea kupanuka. Badala ya fungu la aina ya binadamu kuwa bora, hao watawala walio kama jua katika mifumo hiyo wakaanza ‘kuunguza aina ya binadamu kwa joto kubwa.’ Vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Hispania, Ethiopia, na Manchuria viliongoza kwenye vita ya ulimwengu ya pili. Historia ya ki-siku-hizi hurekodi kwamba Mussolini, Hitla, na Stalini wakiwa madikteta wakawa na daraka la moja kwa moja na lisilo la moja kwa moja la vifo vya makumi ya mamilioni, kutia ndani wengi wa wanataifa wao wenyewe. Hivi majuzi zaidi, mipambano ya kimataifa au ya wenyewe kwa wenyewe ‘imeunguza’ watu wa nchi kama vile Vietnamu, Kampuchea, Irani, Lebanoni, na Ailandi, pamoja na mabara mengine katika Amerika ya Kilatini na Afrika. Ongezea hayo ule mng’ang’ano wenye kuendelea kati ya mataifa yenye nguvu zaidi, ambayo silaha zayo za nyukilia zenye kutia hofu sana zinaweza kuteketeza aina ya binadamu yote.

  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Leo Hitla na Mussolini, madikteta wenye amri peke yao, wanatisha amani ya ulimwengu kwa ujumla, na wanaungwa mkono kikamili na jamii ya mapadri wa Katoliki ya Roma katika uharibifu wao wa uhuru.”—Fascism or Freedom, 1939, ukurasa 12.

      “Muda wote wa historia sera iliyofuatwa na madikteta wa kibinadamu imekuwa, Tawala au angamiza! Lakini kirekebi cha kutumiwa sasa na Mfalme aliyewekwa na Mungu, Yesu Kristo, kwenye dunia yote, ni, Tawalwa au uangamizwe.”—When All Nations Unite Under God’s Kingdom, 1961, ukurasa 23.

      “Tangu 1945 zaidi ya watu milioni 25 wameuawa katika vita 150 vilivyopiganwa kuzunguka dunia.”—Mnara wa Mlinzi, Julai 1, 1980, ukurasa 6.

      “Mataifa kuuzunguka ulimwengu . . . hayajali sana daraka la kimataifa au amri za mwenendo. Ili kutimiza miradi yao, mataifa mengine yana maoni ya kwamba yana haki kabisa kutumia njia zo zote yanazoziona kuwa lazima—kuchinja watu kwa wingi, kuua, kuteka nyara, kulipua makombora, na kadhalika . . . Ni kwa muda gani mataifa yataendelea kuvumiliana katika mwendo huo wa upumbavu na usiofaa?”—Mnara wa Mlinzi, Julai 15, 1985, ukurasa 4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki