Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jiji Kubwa Lateketezwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Fikiria yaliyotokea miaka sita baadaye. Katika Oktoba 3, 1935, Italia ilivamia Abisinia, ikidai kwamba lilikuwa “bara la kishenzi ambalo lilikuwa lingali linazoea utumwa.” Ni nani, kwa kweli, aliyekuwa wa kishenzi? Je! Kanisa Katoliki lililaumu vikali ushenzi wa Mussolini? Ingawa papa alitoa taarifa zisizoeleweka, maaskofu wake walisema wazi kabisa katika kubariki majeshi yenye silaha ya Italia “bara-baba” lao. Katika kitabu The Vatican in the Age of the Dictators, Anthony Rhodes huripoti hivi:

      15 “Katika Barua ya Uchungaji yake ya Oktoba 19 [1935], Askofu wa Udine [Italia] aliandika, ‘Si la wakati unaofaa wala lenye kufaa kwa sisi kutamka yanayofaa na yasiyofaa ya kisa hiki. Wajibu wetu tukiwa Waitalia, na hata hivyo zaidi tukiwa Wakristo ni kuchangia fanikio la silaha zetu.’ Askofu wa Padua aliandika katika Oktoba 21, ‘katika hizi saa ngumu ambazo sisi tunazipitia, sisi tunawaomba nyinyi mwe na imani katika watawala wetu na majeshi yenye silaha.’ Oktoba 24, Askofu wa Kremona aliweka wakfu bendera kadhaa za kijeshi na akasema: ‘Baraka ya Mungu na iwe juu ya askari-jeshi hawa ambao, juu ya udongo wa Kiafrika, watashinda mabara mapya na yenye rutuba kwa ajili ya ubunifu wa Italia, na hivyo kuwaletea utamaduni wa Kiroma na Kikristo. Italia na isimame kwa mara nyingine tena ikiwa mshauri wa ulimwengu kwa ujumla.’”

      16 Abisinia ikatwaliwa kinguvu, kwa baraka ya makasisi wa Katoliki ya Roma. Je! yeyote wa hawa angeweza kudai, katika maana yoyote, kwamba wao walikuwa kama mtume Paulo katika kuwa ‘bila hatia ya damu ya watu wote’?

      17. Hispania ilitesekaje kwa sababu ya viongozi wa kidini wayo kushindwa ‘kufua panga zao ziwe majembe ya plau’?

      17 Ongezea Ujeremani, Italia, na Abisinia taifa jingine ambalo limekuwa jeruhi kwa uasherati wa Babuloni Mkubwa—Hispania. Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe ya 1936-39 katika bara hilo, kwa sehemu, ilianzishwa kwa sababu ya serikali ya kidemokrasi kuchukua hatua ya kupunguza nguvu kubwa mno za Kanisa Katoliki la Roma. Vita hiyo ilipoanza, Franko, kiongozi Mfashisti Mkatoliki wa majeshi ya Kimapinduzi, alijieleza mwenyewe kuwa “Jenerali Mkuu wa Kikristo wa Krusedi Takatifu,” jina la cheo ambalo baadaye aliacha. Mamia ya maelfu kadhaa ya Wahispania walikufa katika kupigana. Mbali na hilo, kulingana na kadirio dogo, Wateteaji wa Taifa wa Franko walikuwa wameua kimakusudi wanachama 40,000 wa Popular Front, hali hao wa pili nao walikuwa wameua kimakusudi makasisi—watawa wa kiume, mapadri, watawa wa kike, na makasisi wapya 8,000. Hilo ndilo ogofyo na msiba wa vita ya wenyewe kwa wenyewe, ikionyesha hekima ya kutii maneno haya ya Yesu: “Rudisha upanga wako mahali pao, kwa maana wale wote ambao huchukua upanga watapotelea mbali kwa upanga.” (Mathayo 26:52, NW) Ni jambo lenye kunyarafisha kama nini kwamba Jumuiya ya Wakristo hujiingiza katika umwagaji-damu mkubwa hivyo! Kweli kweli viongozi wayo wa kidini wameshindwa kabisa kabisa ‘kufua panga zao ziwe majembe ya plau’!—Isaya 2:4, NW.

  • Jiji Kubwa Lateketezwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku katika ukurasa wa 263]

      “Wafalme . . . Walifanya Uasherati na Yeye”

      Mapema katika miaka ya 1800 wauza-bidhaa wa Ulaya walikuwa wakiingiza kimagendo ndani ya China viasi vikubwa vya kasumba. Katika Machi 1839 maofisa Wachina walijaribu kukomesha uchuuzi huo usio halali kwa kukamata masanduku 20,000 ya dawa hiyo ya kulevya kutoka kwa wauza-bidhaa Waingereza. Hili liliongoza kwenye wasiwasi kati ya Uingereza na China. Mahusiano kati ya nchi hizo mbili yalipozorota, baadhi ya wamisionari Waprotestanti walihimiza Uingereza kwenda vitani, kwa taarifa kama hizi zifuatazo:

      “Jinsi magumu haya yanavyoshangilisha moyo wangu kwa sababu mimi nafikiri huenda serikali ya Uingereza ikakasirishwa vikali, na Mungu, katika nguvu Zake huenda akavunjavunja migogoro inayozuia gospeli ya Kristo isiingie China.”—Henrietta Shuck, misionari wa Baptisti ya Kusini.

      Hatimaye, vita ikafyatuka—vita ambayo leo hujulikana kuwa Vita ya Kasumba. Kwa moyo wote wamisionari walichochea Uingereza kwa maelezo kama haya:

      “Mimi nalazimika kutazama nyuma juu ya hali ya sasa ya mambo sana sana si kuwa ni shauri la kasumba au la Uingereza, kuwa ndilo kusudi kubwa la Mwelekezo wa Kimungu ili kufanya uovu wa mwanadamu utii makusudi Yake ya rehema kuelekea China katika kupenya ukuta wayo wa kujitenga.”—Peter Parker, misionari Mkongrigeshonali.

      Misionari mwingine Mkongrigeshonali, Samuel W. Williams, aliongeza hivi: “Mkono wa Mungu ni wazi katika yale yote ambayo yamefanyika kwa jinsi ya kutokeza, na sisi hatutii shaka kwamba Yeye ambaye alisema alikuja kuleta upanga juu ya dunia amekuja hapa na kwamba ni kwa ajili ya uharibifu mwepesi wa maadui Wake na kusimamishwa kwa ufalme Wake. Yeye atapindua na kupindua mpaka Yeye awe amemthibitisha Mwana-Mfalme wa Amani.”

      Kwa mintarafu ya chinjo lenye kuogofya la wanataifa Wachina, misionari J. Lewis Shuck aliandika: “Mimi huona mandhari kama hizo . . . kuwa ala za Bwana za moja kwa moja katika kuondolea mbali takataka ambayo inazuia usongaji mbele wa Ukweli wa Kimungu.”

      Misionari Mkongrigeshonali Elijah C. Bridgman aliongeza: “Mara nyingi Mungu ametumia mkono imara wa mamlaka ya kiserikali ili kutayarisha njia kwa ajili ya ufalme Wake . . . Chombo katika nyakati hizi zenye maana ni cha kibinadamu; nguvu yenye kuelekeza ni ya kimungu. Gavana mkuu wa mataifa yote ametumia Uingereza kuadhibu na kunyenyekeza China.”—Manukuu yamechukuliwa kutoka “Ends and Means,” 1974, insha ya Stuart Creighton Miller iliyotangazwa katika The Missionary Enterprise in China and America (Durusi la Harvard lililohaririwa na John K. Fairbank).

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki