Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Chavuo Balaa au Muujiza?
    Amkeni!—2003 | Julai 22
    • Mfano mmoja ni aina ya okidi inayokua Australia Magharibi. Ua la okidi hiyo lina petali ambayo, hata kwa binadamu, hufanana kabisa na nyigu mnene wa kike asiye na mabawa. Ua hilo hata hutoa kemikali inayovutia nyigu wa kiume kama ile ambayo hutolewa na nyigu halisi wa kike! Juu ya nyigu huyo bandia kuna vifuko vyenye kunata vilivyojaa chavuo.

      Nyigu wa kiume akivutiwa na harufu ya kemikali hiyo bandia, humkamata nyigu huyo bandia na kujaribu kuruka “naye.” Hata hivyo, anapoondoka, mwendo wake humgeuza yeye pamoja na mwenzake na kumwingiza kwenye vile vifuko vyenye kunata vya chavuo. Baada ya kugundua kosa lake, nyigu wa kiume humwachilia yule nyigu bandia, ambaye huwa ameungana na ua hilo kwa njia inayomwezesha kurudi mahali pake, kisha nyigu huyo wa kiume huruka na kwenda zake, lakini baadaye hujikuta akiwa amepumbazwa tena na ua lingine la okidi. Hata hivyo, yeye huchavusha okidi hiyo kwa chavuo alizobeba kutoka katika ua la kwanza.

      Lakini ikiwa manyigu halisi wa kike wanapatikana, manyigu wa kiume huchagua mmoja wao badala ya yule nyigu bandia. Kwa kufaa basi, okidi huchanua maua yake majuma kadhaa kabla ya manyigu wa kike kuibuka kutoka katika hali yao ya kuwa mabuu ardhini, na hivyo maua hayo hufaidika kwa muda.

  • Chavuo Balaa au Muujiza?
    Amkeni!—2003 | Julai 22
    • [Picha katika ukurasa wa 26]

      Sehemu ya okidi inayofanana na nyigu wa kike

      [Hisani]

      Hammer orchid images: © BERT & BABS WELLS/OSF

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki