-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Kuelekea Juu Kwenye Pwani ya Afrika Mashariki
Mapema sana katika karne ya 20, baadhi ya vichapo vya C. T. Russell vilikuwa vimeenezwa katika sehemu ya kusini-mashariki mwa Afrika na watu mmoja-mmoja waliokuwa wamekubali mawazo machache ya vitabu hivyo lakini walikuwa wameyachanganya na falsafa zao wenyewe. Matokeo yakawa zile zilizoitwa eti harakati za Watchtower ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na Mashahidi wa Yehova. Baadhi yazo zilikuwa na maelekeo ya kisiasa, zikichochea msukosuko miongoni mwa Waafrika wenyeji. Kwa miaka mingi ile sifa mbaya ya vikundi hivyo ilitokeza vizuizi kwa kazi ya Mashahidi wa Yehova.
-
-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Baadhi ya wakuu wa serikali wasiopendelea upande wowote hawakukubali bila kuuliza maswali yale mashtaka ya kikatili yaliyofanywa na makasisi wa Jumuiya ya Wakristo dhidi ya Mashahidi. Ndivyo ilivyokuwa kwa habari ya kamishna wa polisi katika Nyasaland (sasa ni Malawi) aliyejifanya asiweze kutambulika akaenda kwenye mikutano ya Mashahidi wenyeji ili apate kujionea mwenyewe walikuwa watu wa aina gani. Alivutiwa vizuri. Wakati kibali kilipotolewa na serikali ili kuwa na mwakilishi Mzungu mkazi, Bert McLuckie na baadaye ndugu yake Bill walitumwa huko katika miaka ya katikati ya 1930. Waliendelea kuwasiliana na polisi na makamishna wa wilaya ili maofisa hao waweze kuwa na uelewevu ulio wazi wa utendaji wao na ili wasichanganyikiwe kati ya Mashahidi wa Yehova na yoyote ya zile harakati ziitwazo Watchtower kibandia.
-