-
Wanyama Wakubwa wa BahariniAmkeni!—2009 | Desemba
-
-
Ingawa ngisi-jitu na nyangumi huyo anayeitwa sperm ni wakubwa sana, nyangumi wa rangi ya bluu-kijivu, ambaye ndiye mnyama mkubwa zaidi kati ya wanyama wanaonyonyesha, anawazidi kwa ukubwa. Nyangumi wa kike wa aina hiyo mwenye urefu wa mita 33 aliyevuliwa huko Antaktika ndiye nyangumi mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa. Nyangumi wa rangi ya bluu-kijivu anaweza kuwa na uzito wa tani 150 hivi. Uzito wa ulimi wake peke yake ni sawa na uzito wa tembo aliyekomaa! Hebu wazia—nyangumi huyo huzaa mtoto mwenye uzito wa tani tatu na urefu wa mita 7 hadi 8! Kwa sababu ya kuvuliwa sana na wavuvi wa nyangumi, nyangumi huyo karibu atoweke katika miaka ya 1960 na leo amewekwa katika orodha ya wanyama walio katika hatari kubwa ya kutoweka.
-
-
Wanyama Wakubwa wa BahariniAmkeni!—2009 | Desemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 17]
Nyangumi wa rangi ya bluu-kijivu na mtoto wake
-