Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Lakini mabawa mawili ya tai akapewa mwanamke, ili yeye apate kuruka kwenda katika jangwa kwenye mahali pake; huko ndiko yeye analishwa kwa wakati na nyakati na nusu wakati mbali na uso wa nyoka.”—Ufunuo 12:13, 14, NW.

  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 24. Ni nini kilichopata Wanafunzi wa Biblia kilichofanana na kukombolewa kwa Waisraeli kutoka Misri?

      24 Vita ya ulimwengu ya kwanza ilipokuwa ikipiganwa, ndugu waaminifu wa Yesu waliendelea na kushuhudu kwao kadiri walivyoweza. Hiyo ilifanywa usoni mwa upinzani ulioongezewa mkazo kutoka Shetani na vibaraka wake wakali. Mwishowe, kushuhudu peupe kwa Wanafunzi wa Biblia karibu kulisimamishwa. (Ufunuo 11:7-10) Hiyo ilikuwa wakati walipopatwa na kituko kama kile cha Waisraeli katika Misri ambao pia walivumilia chini ya uonevu mkubwa. Ikawa ndipo Yehova alipowaleta upesi, kama kwa mabawa ya tai, kwenye usalama katika jangwa la Sinai. (Kutoka 19:1-4) Hali kadhalika, baada ya mnyanyaso mkali wa 1918-19, Yehova alikomboa mashahidi wake, wenye kuwakilisha mwanamke wake, akawaingiza ndani ya hali ya kiroho iliyokuwa salama kwao kama jangwa lilivyokuwa kwa Waisraeli. Hiyo ilikuja ikiwa jibu la sala zao.—Linga Zaburi 55:6-9.

      25. (a) Ni nini alichotokeza Yehova katika 1919, kama alivyotokeza Waisraeli wakiwa taifa jangwani? (b) Ni nani wanaojumlika kuwa taifa hili, nao wameletwa ndani ya nini?

      25 Huko jangwani, Yehova aliwatokeza Waisraeli wakiwa taifa, akiwaandalia kiroho na kimwili. Hali moja na hiyo, kuanzia 1919, Yehova aliitokeza mbegu ya mwanamke ikiwa taifa la kiroho. Hili lisifikiriwe kuwa ule Ufalme wa Kimesiya ambao umekuwa ukitawala kutoka katika mbingu tangu 1914. Badala ya hivyo, washiriki wa hili taifa jipya ni baki la mashahidi wapakwa-mafuta walio duniani, walioletwa ndani ya hali ya kiroho tukufu katika 1919. Wakiwa sasa wanaandaliwa “kipimo cha ugavi wa chakula chao kwa wakati unaofaa,” hao waliimarishwa kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele.—Luka 12:42, NW; Isaya 66:8.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki