Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hekalu Kubwa la Kiroho la Yehova
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
    • 5. Ni nini kilichofananishwa na madhabahu halisi ya hekalu?

      5 Kukubali kwa Mungu kule kutolewa kwa mwili wa Yesu utumiwe ukiwa dhabihu kulimaanisha kwamba, katika maana ya kiroho, madhabahu iliyo kubwa zaidi ya ile iliyokuwa katika hekalu la Yerusalemu ilichukua sehemu ya kwanza. Madhabahu halisi ambapo wanyama walitolewa kwa ajili ya dhabihu ilitangulia kuonyesha madhabahu hiyo ya kiroho, ambayo kwa kweli ilikuwa “mapenzi” au mpango wa Mungu wa kukubali uhai wa Yesu wa kibinadamu ukiwa dhabihu. (Waebrania 10:10) Hiyo ndiyo sababu mtume Paulo aliweza kuwaandikia Wakristo wenzake: “Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.” (Waebrania 13:10) Kwa maneno mengine, Wakristo wa kweli hufaidika kutokana na dhabihu ya kufunika dhambi iliyo bora zaidi, ambayo makuhani Wayahudi walio wengi walikataa.

  • Hekalu Kubwa la Kiroho la Yehova
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
    • Kwa hakika, kuanzia wakati huo maishani mwake na kuendelea, alitimiza maneno ya Zaburi 40:6-8, kama ionyeshwavyo baadaye na mtume Paulo: “Dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari.” (Waebrania 10:5) Kwa njia hiyo Yesu alionyesha kujua kwake kwamba Mungu ‘hakutaka’ dhabihu za wanyama ziendelee kutolewa kwenye hekalu la Yerusalemu. Badala ya hilo, alitambua kwamba Mungu alikuwa amemtayarishia yeye, Yesu, mwili mkamilifu wa kibinadamu, apate kuutoa ukiwa dhabihu. Hilo lingeondoa uhitaji wowote zaidi wa dhabihu za wanyama. Akionyesha tamaa yake yenye kuhisiwa moyoni ya kunyenyekea mapenzi ya Mungu, Yesu aliendelea kusali: “Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu.” (Waebrania 10:7) Ni kielelezo kitukufu kama nini cha moyo mkuu na ujitoaji usio na ubinafsi alichoweka Yesu siku hiyo kwa wote ambao baadaye wangekuwa wanafunzi wake!—Marko 8:34.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki