Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Novemba 1
    • Ni kalamu na wino wa aina gani uliotumiwa nyakati za Biblia?

      Kalamu zilizotengenezwa kwa mafunjo kutoka misri, yapata karne ya kwanza W.K.

      Katika umalizio wa barua ya mwisho kati ya barua zake tatu zilizo katika Biblia, mtume Yohana alisema hivi: “Nilikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sitaki kuendelea kukuandikia kwa wino na kalamu.” Tafsiri ya neno kwa neno ya Kigiriki cha kale ambacho Yohana alitumia inaonyesha kwamba hakutaka kuendelea kuandika kwa kutumia “[wino] mweusi na utete.”—3 Yohana 13, The Kingdom Interlinear Translation of the Greek Scriptures.

  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Novemba 1
    • Aina nyingi za wino, au “mweusi,” zilikuwa mchanganyiko wa masizi ya jiko au taa na mpira wenye kunata, ambao ulitumiwa kama gundi. Wino huo uliuzwa ukiwa mkavu na kabla ya kutumiwa ulipaswa kuchanganywa na kiwango maalumu cha maji. Wino huo ulipotumiwa, ungeonekana tu juu mafunjo au ngozi na haukupenya upande wa pili. Hivyo, mwandishi angeweza kufuta kwa urahisi kosa lolote kwa kutumia sifongo yenye unyevunyevu, ambayo ilikuwa mojawapo ya vifaa muhimu vya mwandishi. Habari hizo kuhusu wino uliotumiwa zamani, zinaonyesha kile ambacho waandikaji wa Biblia walikuwa wakifikiria walipoandika kuhusu kuondolewa au kufutwa kwa majina kutoka katika kitabu cha kumbukumbu cha Mungu.—Kutoka 32:32, 33; Ufunuo 3:5, Kingdom Interlinear.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki