Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Karibu wakati huo, Llewelyn Phillips, kutoka ofisi ya tawi ya Rhodesia Kaskazini, alienda Kongo ya Ubelgiji ili kuwatetea Mashahidi waliokuwa wakiteswa. Gavana mkuu na maofisa wengine wa serikali walimsikiliza alipokuwa akiwaeleza kuhusu kazi ya kuhubiri ujumbe wa Ufalme na tofauti iliyopo kati ya mafundisho ya Mashahidi na ya Kitawala.

  • Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (Kinshasa)
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • 1951: Makala nyingi zimechapishwa katika magazeti ya Ubelgiji zikidai kwamba Watch Tower Society na Mashahidi wa Yehova wana uhusiano na “Kitawala,” kikundi chenye siasa kali katika Kongo ya Ubelgiji. Sheria ya Ubelgiji inasema kwamba mtu akijibu makala iliyochapishwa kwenye gazeti, basi ni lazima gazeti hilo lichapishe jibu lake. Tumetumia ifaavyo haki hiyo ili kutetea kazi ya Ufalme kwa kukanusha makala hizo za uwongo, na majibu yetu yamechapishwa.

      Tangu Januari [12], 1949, kazi ya Watch Tower Society imepigwa marufuku katika Kongo ya Ubelgiji na mashahidi wa kweli wa Yehova wameteswa kwa sababu ya ripoti hizo za uwongo. Barua za malalamiko zimeandikwa na kupelekwa kwa waziri wa koloni, na uthibitisho wa kutosha umetolewa kuonyesha kwamba Mashahidi wa Yehova na Watch Tower Society hawana uhusiano wowote na kikundi cha mapinduzi cha “Kitawala,” lakini malalamiko hayo hayajajibiwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki