Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Ezra
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
    • HEKALU LAJENGWA UPYA

      (Ezra 1:1–6:22)

      Kupatana na agizo la kuwekwa huru lililotolewa na Koreshi, Wayahudi 50,000 walio uhamishoni wanarudi Yerusalemu huku wakiongozwa na Gavana Zerubabeli, au Sheshbaza. Watu hao waliorudishwa wanajenga madhabahu mahali pake na kuanza kumtolea Yehova dhabihu.

      Mwaka unaofuata Waisraeli wanaweka msingi wa nyumba ya Yehova. Maadui wanapinga kazi ya ujenzi na hatimaye wanafanikiwa kupata amri ya kifalme ili kusimamisha kazi hiyo. Nabii Hagai na Zekaria wanawachochea watu waendelee na ujenzi wa hekalu licha ya marufuku. Maadui wao wanaogopa kupinga lile agizo la Uajemi lisiloweza kubatilishwa ambalo Koreshi alitoa na hivyo wananyamazishwa. Uchunguzi rasmi unafunua kwamba Koreshi alitoa agizo “kuhusu nyumba ya Mungu katika Yerusalemu.” (Ezra 6:3) Kazi inasonga mbele vizuri na kukamilika.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Ezra
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
    • 3:8-10; 4:23, 24; 6:15, 16—Ilichukua miaka mingapi kujenga upya hekalu? Msingi wa hekalu uliwekwa mwaka wa 536 K.W.K., “mwaka wa pili wa kuja kwao.” Kazi ya ujenzi ilisimama katika siku za Mfalme Artashasta, mwaka wa 522 K.W.K. Marufuku yaliendelea hadi mwaka wa 520 K.W.K., mwaka wa pili wa Mfalme Dario. Hekalu lilikamilishwa katika mwaka wa sita wa utawala wake, au mwaka wa 515 K.W.K. (Ona sanduku lenye kichwa “Wafalme wa Uajemi Kuanzia Mwaka wa 537 Hadi 467 K.W.K.”) Hivyo, ujenzi wa hekalu ulichukua miaka 20 hivi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki