-
Kidingapopo—Tisho LinaloongezekaAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
Hii ni kwa sababu mbu anayeitwa Aedes wa kike hutaga mayai yake mahali palipo na maji ambayo hayasongi.b Kwa kuwa watu katika Amerika ya Latini na ya Karibea hukusanya na kuhifadhi maji ndani ya matangi yaliyotengenezwa kwa saruji, wataalamu wa afya wanawasihi wafunike matangi hayo. Hilo huzuia matangi hayo yasiwe maeneo ya mbu ya kutagia mayai. Pia, watu wanaweza kudhibiti kuenea kwa mbu hao wanapodumisha ua ukiwa safi kwa kuondoa magurudumu ya gari ya zamani, mikebe, nyungu za maua, vyombo vya plastiki—chochote kinachoweza kuzuia maji yasisonge.
-
-
Kidingapopo—Tisho LinaloongezekaAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
Unaweza kufanya nini ili uepuke kuumwa na mbu? Vaa shati lenye mikono mirefu, suruali au rinda refu, na utumie dawa za kufukuza mbu. Ingawa mbu wanaweza kuuma wakati wowote, wao huwa wengi sana saa mbili kabla ya jua kutua na baada ya jua kuchomoza. Pia, kulala ndani ya neti yenye dawa inayofukuza mbu ni kinga.
-
-
Kidingapopo—Tisho LinaloongezekaAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
[Mchoro katika ukurasa wa 25]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Hakikisha Hakuna Maeneo Ambayo Mbu Wanaweza Kutaga Mayai
1. Magurudumu yaliyotupwa
2. Michirizi ya maji ya mvua
3. Nyungu za maua
4. Vyombo vya plastiki
5. Mapipa na mikebe iliyotupwa
Usikae Mahali Palipo na Mbu Wengi
a. Vaa shati lenye mikono mirefu, suruali au rinda refu. Tumia dawa za kufukuza mbu
b. Lala ndani ya neti
-