Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Manufaa za Misitu ya Mvua
    Amkeni!—1998 | Mei 8
    • “Miti ya [West] Indies ni kitu ambacho hakiwezi kuelezeka, kwa sababu ya wingi wake,” Gonzalo Fernández de Oviedo mwandika-matukio Mhispania akasema kwa mshangao katika mwaka wa 1526. Karne tano baadaye kadirio lake la thamani lingali sahihi. “Msitu wa mvua,” aandika mwandikaji Cynthia Russ Ramsay, ni “wenye unamna mwingi, wenye utata, na mfumikolojia usioeleweka sana katika dunia.”

      Mwanabiolojia wa kitropiki Seymour Sohmer ataarifu: “Hatupaswi kamwe kusahau uhakika wa kwamba twajua machache sana au hatujui lolote kuhusu jinsi ambavyo misitu mingi yenye unyevu ya kitropiki imeundwa na jinsi ifanyavyo kazi, bila kutaja spishi zilizo ndani yake.” Idadi kubwa sana ya spishi na utata wa uhusiano wake hufanya kazi ya mtafiti kuwa yenye kukatisha tamaa.

      Msitu ulio katika maeneo yenye joto la wastani huenda ukawa tu na spishi chache za miti katika kila eka. Kwa upande ule mwingine, eka moja ya msitu wa mvua, yaweza kuwa na spishi tofauti-tofauti 80, hata ingawa jumla ya idadi ya miti kwa kila eka kwa wastani ni karibu 300 tu. Kwa kuwa uainishaji wa hali kama hiyo ya kuwa na unamna-namna ni kazi ya kuchosha na yenye kuhitaji uangalifu wenye bidii, ni visehemu vichache tu vya msitu wa mvua ambavyo vimeweza kuchanganuliwa. Hata hivyo, vile ambavyo vimechanganuliwa, hutoa matokeo yenye kushangaza.

      Miti ya namna nyingi huandaa makao yasiyohesabika yanayotoa mambo yahitajikayo kwa ajili ya kuendelea kuwako kwa spishi kwa ajili ya idadi kubwa ya wakazi wa msituni—nyingi sana kuliko ilivyoweza kuwaziwa. Chuo cha Kitaifa cha Sayansi cha Marekani chasema kwamba eneo lifananalo na hilo la kilometa kumi za mraba za eneo la msitu wa mvua wa zamani laweza kuwa na spishi tofauti-tofauti 125 za mamalia, spishi 100 za wanyama-watambazi, spishi 400 za ndege, na spishi 150 za vipepeo. Kwa kulinganisha, twaona ya kwamba Amerika Kaskazini yote imetembelewa na spishi zipunguazo 1,000 tu za ndege.

      Ingawa baadhi ya mamiriadi ya spishi za mimea na wanyama zaweza kupatikana katika sehemu kubwa ya msitu wa mvua, nyingine ziko tu katika safu moja ya milima. Hilo ndilo huzifanya ziwe rahisi kudhuriwa. Kufikia wakati wakataji-miti walipomaliza kufyeka safu moja ya misitu katika Ekuado miaka michache iliyopita, spishi 90 za kienyeji zilikuwa tayari zimetoweka.

      Kwa kukabili misiba kama hiyo, shirika la United States Interagency Task Force on Tropical Forests laonya hivi: “Jumuiya ya mataifa yapaswa kuanzisha upesi shambulio lililoharakishwa na lenye umoja kuhusu tatizo hilo ikiwa mali hizi zilizoshushiwa thamani na ambazo huenda zisiweze kurudishwa tena zapasa kulindwa dhidi ya kuharibiwa kikweli kufikia mapema mwa karne ijayo.”

  • Manufaa za Misitu ya Mvua
    Amkeni!—1998 | Mei 8
    • Mwanadamu hawezi kuthubutu kupuuza chanzo cha ugavi wake wa chakula. Mimea na wanyama wa kufugwa waweza kudhoofishwa kwa uzalishaji unaopita kiasi baina ya spishi za nasaba moja. Msitu wa mvua, ukiwa na wingi wa spishi, waweza kuandaa unamna-namna wa kijeni unaohitajiwa ili kuimarisha mimea hii au wanyama. Kwa kielelezo, mwanabotania Mmexico Rafael Guzmán aligundua spishi mpya za nyasi zinazohusiana na mahindi ya kisasa. Ugunduzi wake uliwasisimua wakulima kwa sababu nyasi hii (Zea diploperennis) hukinza magonjwa makubwa tano kati ya yale saba ambayo hushambulia mahindi. Wanasayansi wanatumainia kutumia spishi hiyo mpya ili kutokeza namna nyingi za mahindi zenye kukinza ugonjwa.

      Katika mwaka wa 1987 serikali ya Mexico ilihami safu ya milima ambako mahindi hayo ya msituni yalipatikana. Lakini kukiwa na msitu mkubwa sana unaoangamizwa, hakuna shaka kwamba spishi zenye thamani kama hii zinapotezwa, hata kabla hazijajulikana. Katika msitu wa Kusini-Mashariki mwa Asia, kuna spishi kadhaa za ng’ombe wa msituni ambazo zingeweza kuimarisha uzao wa ng’ombe wa kufugwa. Lakini spishi hizi zote ziko ukingoni mwa kuangamizwa kwa sababu ya kuharibiwa kwa makao yao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki