Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mfumo Tata wa Viumbe
    Amkeni!—2001 | Novemba 22
    • Je, Twahitaji Aina Zote Hizo?

      Je, kuna haja ya kuhangaikia kuangamia kwa aina mbalimbali za viumbe? Je, kweli twahitaji aina tofauti-tofauti za viumbe? Wataalamu wengi wanaoheshimiwa husisitiza kwamba twahitaji aina hizo. Aina za viumbe duniani huwaandalia wanadamu chakula, kemikali muhimu, na bidhaa na huduma nyinginezo. Pia, fikiria kuhusu faida zinazoweza kutokana na aina ambazo hazijagunduliwa. Kwa mfano, imekadiriwa kwamba dawa 120 kati ya dawa 150 kuu ambazo madaktari huwapendekezea watu nchini Marekani, hutengenezwa kwa mali asili. Hivyo, aina za mimea zinapoangamia, wanadamu hupoteza njia ya kuvumbua dawa na kemikali mpya. Bwana Ghillean Prance, mkurugenzi wa Bustani za Kew huko London, alisema hivi: ‘Kila mara aina moja ya kiumbe inapoangamia, tunapoteza kitu ambacho tungetumia siku za baadaye. Tunapoteza dawa inayoweza kutibu UKIMWI, au zao linaloweza kukinza virusi. Hivyo, ni lazima tukomeshe uharibifu wa viumbe, si kwa faida ya dunia tu bali kwa ajili ya . . . mahitaji na matumizi yetu.’

      Pia, twahitaji mazingira yanayoweza kudumisha uhai wa viumbe vyote. Mazingira yasiyo na kasoro hutimiza kazi muhimu kama vile kutengeneza oksijeni, kusafisha maji, kuondoa vichafuzi, na kuzuia mmomonyoko wa udongo.

      Wadudu huchavusha mimea. Vyura, samaki, na ndege huangamiza wadudu waharibifu; kome na viumbe vingine vinavyoishi majini husafisha maji; mimea na vijidudu hutengeneza udongo. Huduma hizo hutokeza faida kubwa sana za kiuchumi. Kulingana na kadirio la kiwango cha chini lililofanywa kupatana na bei za 1995, aina mbalimbali za viumbe ulimwenguni pote huleta faida ya dola bilioni 3,000 za Marekani kila mwaka.

  • Ni Nini Kitakachotokea Wakati Ujao?
    Amkeni!—2001 | Novemba 22
    • Mwanasayansi Anthony C. Janetos, aliandika hivi katika gazeti la Consequences: “Watu wengi watakubali kwamba tukiwa jamii tuna wajibu wa kimaadili wa kulinda dunia ili iweze kukalika, na kutunza unamna-namna wake wa viumbe kwa faida ya sasa ya wanadamu na ya wakati ujao. Ili tuweze kufanya hivyo twapaswa kuelewa umuhimu wa kuwa na aina mbalimbali za viumbe—jinsi zinavyonufaisha mazingira na jinsi tunavyoweza kuzitumia—na kujitoa mhanga kuzihifadhi.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki