-
Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi UliopoJe, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 22]
“Hali za kipekee zilizo duniani ambazo zimetokezwa na ukubwa wake ufaao, mfanyizo wake ufaao wa elementi, na kuwa kwake na mzunguko ambao karibu uwe duara kabisa na umbali ufaao kabisa kutoka kwenye nyota yenye kudumu, yaani jua, zimefanya maji yaweze kurundamana kwenye uso wa dunia.” (Integrated Principles of Zoology, chapa ya 7) Uhai duniani haungeweza kutokea bila maji.
-
-
Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi UliopoJe, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
Hali za Dunia Zenye Kufaa Sana
Mambo mengine yaliyopimwa kwa usahihi kabisa yanahitajiwa ili tuweze kuishi. Ebu fikiria vipimo vya dunia na mahali ilipo kwa kulinganisha na mfumo wetu wa jua na sayari zake. Kitabu cha Biblia cha Ayubu chauliza maswali haya yenye kunyenyekeza: “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? . . . Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?” (Ayubu 38:4, 5) Maswali hayo yanataka jibu wakati huu kuliko wakati mwingine wowote. Kwa nini? Kwa sababu ya mambo ya ajabu ambayo yamegunduliwa kuhusu dunia yetu—kutia ndani ukubwa wake na mahali ilipo katika mfumo wetu wa jua.
Hakuna sayari iliyo kama dunia yetu ambayo imewahi kupatikana mahali pengine popote katika ulimwengu. Ni kweli kwamba wanasayansi fulani huelekezea uthibitisho usio wa moja kwa moja kwamba nyota fulani zinazungukwa na vitu ambavyo ni vikubwa kuliko dunia yetu kwa mamia ya mara. Ingawa hivyo, dunia yetu ina ukubwa ufaao kabisa maisha yetu. Kwa maana gani? Ikiwa dunia ingalikuwa kubwa kidogo tu, nguvu yake ya uvutano ingalikuwa nyingi zaidi na hiyo ingefanya hidrojeni, ambayo ni hewa nyepesi, ijikusanye, ikinaswa na uvutano wa dunia. Kwa hiyo, angahewa halingeweza kudumisha uhai. Kwa upande mwingine, ikiwa dunia yetu ingalikuwa ndogo kidogo tu, oksijeni yenye kudumisha uhai ingeponyoka na maji yote yangekuwa mvuke. Katika hali hizo zote mbili, hatungeweza kuishi.
Pia, dunia ipo umbali ufaao zaidi kutoka kwenye jua, jambo ambalo ni muhimu kwa uhai kusitawi. Mtaalamu wa nyota John Barrow na mtaalamu wa hesabu Frank Tipler walichunguza “ulinganisho wa nusu-kipenyo ya Dunia na umbali kutoka kwenye Jua.” Wao walikata kauli kwamba wanadamu hawangeweza kuishi “iwapo ulinganisho huo ungekuwa tofauti kidogo na jinsi ulivyo sasa.” Profesa David L. Block asema: “Hesabu inaonyesha kwamba kama dunia ingalikuwa karibu na jua kwa asilimia 5 tu, joto jingi kupita kiasi lingetukia miaka milioni 4 000 iliyopita. Ikiwa, kwa upande mwingine, dunia ingalikuwa mbali zaidi na jua kwa asilimia 1 tu, barafu nyingi zingalifunika dunia miaka ipatayo milioni 2 000 iliyopita.”—Our Universe: Accident or Design?
Kwa kuongezea usahihi huo, unaweza kuongezea jambo la kwamba dunia huzunguka kwenye mhimili wake mara moja kwa siku, kwa mwendo ufaao ili kutokeza hali-joto za kiasi. Sayari ya Zuhura huchukua siku 243 ili kuzunguka kwenye mhimili wake. Ebu wazia kama dunia ingalichukua muda mrefu hivyo kuzunguka! Hatungeweza kuokoka joto kali sana na baridi kali sana ambazo zingetokana na siku ndefu sana na usiku mrefu sana.
Jambo jingine dogo lililo muhimu ni njia ya dunia yetu kulizunguka jua. Nyota-mkia zina njia pana zenye umbo la yai. Kwa uzuri, sivyo ilivyo na dunia. Mzunguko wake ni karibu uwe duara kabisa. Tena hii inatuzuia tusipatwe na joto kali sana au baridi kali sana.
-