Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuwaandalia Watoto Mahitaji Yao
    Amkeni!—2003 | Desemba 22
    • Ni Jambo la Kawaida

      Akina mama fulani vijana huhuzunika na kuhisi uchovu majuma machache ya kwanza baada ya kupata mtoto. Hata wanawake ambao walitaka sana kuwa na mtoto wanaweza kusononeka. Hilo ni jambo la kawaida. Hiyo ni kwa sababu viwango vya homoni hubadilika-badilika akina mama wanapojifungua. Pia wanawake wanapojifungua kwa mara ya kwanza, wanakuwa na majukumu mbalimbali kama vile kumlisha mtoto, kumbadilisha nepi na kumtunza kila wakati.

      Mama mmoja alihisi kwamba mtoto wake analia ili kumkasirisha tu. Si ajabu kwamba mtaalamu wa masuala ya kulea watoto huko Japan alisema: “Akina mama wote hupata mfadhaiko unaotokana na kulea watoto.” Kulingana na mtaalamu huyo, “ni muhimu mama asijitenge kamwe.”

      Hata mama akishuka moyo wakati fulani, anaweza kumlinda mtoto wake asiathiriwe na hisia zake zinazobadilika-badilika. Gazeti Time linasema: “Akina mama waliojitahidi kuwatunza watoto wao na kucheza nao licha ya kushuka moyo, waliwasaidia watoto wao kuwa wachangamfu.”b

  • Kuwaandalia Watoto Mahitaji Yao
    Amkeni!—2003 | Desemba 22
    • b Iwapo mama ana huzuni nyingi sana, amevunjika moyo, havutiwi na mtoto wake, na hapendezwi na chochote, huenda anaugua ugonjwa wa kushuka moyo baada ya kujifungua. Ikiwa ndivyo, anapaswa kumwona daktari. Tafadhali ona matoleo ya Amkeni! ya Julai 22, 2002, ukurasa 19-23 na Juni 8, 2003, ukurasa wa 21-23.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki