-
Wafuaji wa Nguo Wenye Bidii wa AbidjanAmkeni!—2007 | Juni
-
-
Sabuni ya Mafuta ya Chikichi
Sabuni ni muhimu sana katika kazi ya mfuaji. Hivyo mfuaji mpya hufunzwa pia matumizi yanayofaa ya sabuni ya mafuta ya chikichi. Sabuni za aina tatu hutumiwa, nazo hutofautishwa kwa rangi zake. Sabuni nyeupe na ya manjano hutumiwa kwa nguo ambazo si chafu sana, nayo nyeusi hutumiwa kwa nguo chafu sana. Inakuwa nyeusi kwa sababu ya mafuta ya chikichi ambayo ndiyo kiambato kikuu. Kwa kuwa kila fanico hutumia vipande kumi vya sabuni kila siku, kuna watu wanaotengeneza sabuni karibu nao ambao huwauzia.
Tulitembelea mahali hapo sahili pa kutengenezea sabuni kwenye kilima karibu na mahali pa kufulia nguo. Kazi kubwa ya kutengeneza sabuni huanza saa 12 asubuhi. Tayari wafanyakazi huwa wamenunua vifaa vinavyohitajiwa katika soko la karibu, yaani, mafuta ya chikichi yaliyoganda, potasiamu haidroksaidi, chumvi, umajimaji wa sabuni uliochacha, mafuta ya nazi, na siagi ya kakao. Vitu vyote hivyo vinaweza kuvundishwa kwa bakteria. Wanavichemsha vitu vyote hivyo kwenye moto mkali wa kuni vikiwa kwenye pipa kubwa la chuma. Baada ya kuupika mchanganyiko huo kwa muda wa saa sita hivi, wanaumimina katika sinia na mabakuli na kungoja upoe. Saa kadhaa baadaye wanakata sabuni vipande vikubwa-vikubwa.
Halafu mwenye kutengeneza sabuni hubeba vipande vingi kichwani hadi chini ya kilima walipo fanico. Anawafikishiaje wafuaji sabuni ikiwa wana kazi nyingi ya kufua mtoni? Anateremka ndani ya maji yanayomfikia kiunoni akiwa na sabuni katika bakuli kubwa ya plastiki anayoacha ielee juu ya maji hadi kwa anayehitaji.
-
-
Wafuaji wa Nguo Wenye Bidii wa AbidjanAmkeni!—2007 | Juni
-
-
[Picha katika ukurasa wa 12]
Mtengenezaji wa sabuni akiuza vipande vya sabuni
-