Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wajue Nyuki Wasiouma wa Australia
    Amkeni!—2000 | Novemba 8
    • Mizinga ya nyuki wasiouma ni tofauti sana na ile ya nyuki wengine wanaotoa asali. Hata, mara nyingi huitwa viota. Badala ya kuhifadhi asali na chavuo katika sega la asali la kawaida lenye pande sita, nyuki wasiouma hutengeneza vitundu vingi vyenye umbo la yai. Vitundu hivyo hufunikwa vikisha jaa, halafu vitundu vingine hutengenezwa juu yake au kando yake.

      Ndani ya Kiota

      Acheni tuchunguze kiota, makao ya nyuki wasiouma wapatao 15,000. Lakini, uwe mwangalifu kwa kuwa nyuki hao wanaweza kukuuma kidogo kwa taya zao ingawa hawaumizi.

      Pembeni mwa kiota hicho twaona utendaji mkubwa ajabu. Nyuki hao wanafanya kazi kwa umoja kabisa. Kila mmoja wao anafahamu barabara jambo la kufanya na mahali pa kulifanyia. Twaona nyuki mmoja mdogo akilainisha na kung’arisha kitundu kipya cha asali, kana kwamba anaiga kwa usahihi kabisa mchoro fulani. Kando yetu nyuki wanne zaidi wanafunika kitundu ambacho kimetoka tu kujazwa asali. Kiambaza chenye pande tatu hutumiwa kama fremu inayotegemeza vitundu vya asali. Uhandisi huu bora kabisa hutegemeza uzito wa asali.

      Sasa twaingia chumba cha pili nasi twaona nyuki mmoja aliye mkubwa kuliko nyuki wengine. Huyu ndiye malkia mwenye fahari tosha! Anapendeza kama nini, akiwa na rangi nyeusi-nyangavu na duara za kidhahabu huku akiwa amezingirwa na kundi kubwa la nyuki wengine wenye shughuli nyingi! Sasa malkia aanza kutaga mayai katika vijumba 60 alivyotayarishiwa. Anataga kwa ustadi na kwa uangalifu mkubwa kama nini, anashabihi mama anayemlaza mtoto wake mchanga kitandani! Angalia pia namna wafanyakazi wanavyofunika hima-hima vijumba hivyo baada ya malkia kutaga mayai ndani yake. Kazi hiyo yakamilika baada ya dakika chache tu.

  • Wajue Nyuki Wasiouma wa Australia
    Amkeni!—2000 | Novemba 8
    • Nyakati nyingine, nyuki mmoja mpelelezi hutumwa kwenda kutafuta shimo linalofaa kujengwa kiota. Kisha “wahandisi” huja kukagua mahali hapo. Kwa kawaida wataalamu 30 hadi 50 hukagua ndani ya shimo hilo kwa saa kadhaa, kana kwamba wanachora plani ya nyumba kwa mistari na vijiti. Halafu, wakisha amua kwamba msingi huo unafaa, wanarejea nyumbani ili kutoa ripoti. Kisha, kwa kawaida katika muda wa saa 48, “wajenzi” wenyewe huwasili. Kundi hilo laweza kuwa na zaidi ya nyuki elfu moja—lakini halina malkia. Upesi wanaanza kazi, wakileta vifaa vya ujenzi na chakula kutoka kwa kiota cha awali.

      Ili kutayarisha chumba cha malkia kwenye kiota hicho kipya, ni sharti chumba cha kutagia mayai kijengwe kwa hali ya kuweza kudumisha halijoto inayofaa—ya nyuzi Selsiasi 28 hivi. Ili kutimiza takwa hilo, nyuki wafanyakazi hulazimika kufunika kiota chote kwa cerumen, kana kwamba wanafunika kiota kwa blanketi. Ni kana kwamba nyuki hao wenye hekima wanajua kuwa ni lazima mayai yapashwe joto.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki