-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1992 | Februari 1
-
-
Hata hivyo, wana-wafalme Wamisri hawakufanya mapatano yeyote pamoja na Abrahamu ili Farao amwoe Sara. Walimleta Sara mwenye kupendeza ndani ya nyumba ya Farao tu, na mtawala wa Misri akampa zawadi Abrahamu, aliyedhaniwa kuwa ndugu yake. Lakini baada ya hilo, Yehova aliipiga nyumba ya Farao mapigo. Hali ya kweli ilipofunuliwa kwa Farao katika njia isiyotajwa, alimwambia Abrahamu hivi: “Mbona ulisema, Huyu ni umbu langu [dada yangu, NW] hata nikamtwaa [nikawa karibu kumtwaa, NW] kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako”!—Mwanzo 12:14-19.
Union Version na tafsiri nyinginezo za Biblia hufasiri sehemu hiyo ya italiki iliyo juu ya mstari huo “hata nikamtwaa kuwa mke wangu” au katika maneno kama hayo. Hata ingawa si fasiri isiyo sahihi, mpangilio wa maneno kama huo waweza kutoa maana kwamba Farao alikuwa kwa kweli amemwoa Sara, kwamba ndoa hiyo ilikuwa uhakika uliotimizwa. Yaweza kuonwa kwamba kwenye Mwanzo 12:19 kitenzi cha Kiebrania kinachofasiriwa “kumtwaa” kimo katika hali ya kutokamilika, inayoonyesha kitendo ambacho hakijamalizika bado. New World Translation hufasiri kitenzi hicho cha Kiebrania kupatana na muktadha na katika njia inayoonyesha wazi hali ya kitenzi hicho—“hata nikawa karibu kumtwaa awe mke wangu.”a Ingawa Farao alikuwa “karibu kumtwaa” Sara awe mke wake, hakuwa bado amemaliza taratibu au sherehe zozote zilizohusika.
Abrahamu amechambuliwa mara nyingi kwa ajili ya jinsi alivyoshughulikia jambo hilo, lakini yeye alitenda kwa ajili ya masilahi ya Mbegu iliyoahidiwa na hivyo kwa ajili ya ainabinadamu yote.—Mwanzo 3:15; 22:17, 18; Wagalatia 3:16.
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1992 | Februari 1
-
-
a Tafsiri ya J. B. Rotherham husomeka hivi: “Mbona ulisema, Yeye ni dada yangu; na kwa hiyo nikawa karibu kumtwaa awe mke wangu?”
-