-
“Mwanamke Bora Sana”Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 1
-
-
“Wewe ni nani, binti yangu?” Naomi akamuuliza Ruthu alipofika nyumbani. Labda aliuliza hivyo kwa sababu kulikuwa na giza, lakini Naomi alitaka pia kujua ikiwa bado Ruthu alikuwa mjane yuleyule au kama sasa alikuwa na tarajio la kuolewa. Ruthu akamweleza haraka mama-mkwe wake mambo yote yaliyokuwa yametukia kati yake na Boazi. Kisha akamwonyesha zawadi ya ukarimu ya shayiri ambayo Boazi alikuwa amemwambia ampe Naomi.d—Ruthu 3:16, 17.
-
-
“Mwanamke Bora Sana”Mnara wa Mlinzi—2012 | Oktoba 1
-
-
d Boazi alimpa Ruthu vipimo sita vya uzito usiojulikana, labda kuonyesha kwamba kama vile siku sita za kufanya kazi zilivyofuatwa na pumziko la Sabato, ndivyo siku za Ruthu za kuteseka akiwa mjane zingefuatwa na “pumziko” ambalo angepata kwa kuwa na nyumba na mume. Kwa upande mwingine, vipimo sita—labda vilivyochotwa kwa sepetu—ndio uzito pekee ambao Ruthu angeweza kubeba.
-