-
“Mwanamke Bora Sana”Igeni Imani Yao
-
-
19, 20. (a) Kwa nini Boazi hakumwoa Ruthu moja kwa moja? (b) Boazi alimwonyeshaje Ruthu fadhili na ufikirio?
19 Boazi aliendelea kusema: “Basi sasa, binti yangu, usiogope. Yote utakayosema nitakufanyia, kwa maana kila mtu aliye katika lango la watu wangu anajua kwamba wewe ni mwanamke bora sana.” (Rut. 3:11) Alipendezwa na wazo la kumwoa Ruthu; labda hakushangaa sana alipoombwa kuwa mkombozi wake. Hata hivyo, Boazi alikuwa mwanamume mwadilifu na hangefanya tu alivyopenda. Alimwambia Ruthu kwamba kulikuwa na mkombozi mwingine ambaye alikuwa mtu wa ukoo wa karibu zaidi wa familia ya Naomi. Boazi angezungumza na mwanamume huyo kwanza na kumpa nafasi ya kuwa mume wa Ruthu.
Kwa sababu Ruthu aliwatendea wengine kwa fadhili na heshima, alijulikana kuwa mwanamke bora
-
-
“Mwanamke Bora Sana”Igeni Imani Yao
-
-
21. Ni nini kilichomsaidia Ruthu ajulikane kuwa “mwanamke bora sana,” na tunawezaje kuiga mfano wake?
21 Kwa kweli, Ruthu aliridhika sana alipotafakari mambo ambayo Boazi alikuwa amemwambia, kwamba alijulikana na watu wote kuwa “mwanamke bora sana”! Bila shaka, tamaa yake ya kutaka kumjua Yehova na kumtumikia ilimsaidia sana ajulikane kwa njia hiyo. Pia, alikuwa amemtendea Naomi na watu wake kwa fadhili na ufikirio sana, akifuata kwa hiari njia na desturi ambazo hakuzijua mwanzoni. Tukiiga imani ya Ruthu, tutajitahidi kuwaheshimu wengine na pia kuheshimu njia na desturi zao. Tukifanya hivyo, huenda sisi pia tukajulikana kuwa watu bora sana.
-