-
Jitahidi Kuwaona Wengine Kama Yehova AnavyowaonaMnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
-
-
Jitahidi Kuwaona Wengine Kama Yehova Anavyowaona
“BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo.”—1 SAMWELI 16:7.
1, 2. Maoni ya Yehova kumhusu Eliabu yalitofautianaje na ya Samweli, na hilo linaweza kutufunza nini?
KATIKA karne ya 11 K.W.K., Yehova alimpa nabii Samweli mgawo wa siri. Alimwagiza nabii huyo aende kwa Yese na kumtia mafuta mmoja wa watoto wake wa kiume ili baadaye awe mfalme wa Israeli. Samweli alipomwona Eliabu, mzaliwa wa kwanza wa Yese, alikuwa na uhakika kwamba amempata mtu ambaye Mungu alikuwa amemchagua. Lakini Yehova akasema: “Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.” (1 Samweli 16:6, 7) Samweli hakumwona Eliabu kama Yehova alivyomwona.a
-
-
Jitahidi Kuwaona Wengine Kama Yehova AnavyowaonaMnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
-
-
a Baadaye ilidhihirika kwamba Eliabu hakuwa na sifa zinazofaa kuwa mfalme wa Israeli hata ingawa alikuwa na sura nzuri. Eliabu pamoja na Waisraeli wengine walijikunyata kwa woga wakati jitu la Wafilisti, Goliathi, lilipowaita Waisraeli wakapigane.—1 Samweli 17:11, 28-30.
-