Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 8/15 kur. 24-26
  • Lile Fumbo la Malango

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Lile Fumbo la Malango
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Mataifa Yakusanyika Megido
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 8/15 kur. 24-26

Lile Fumbo la Malango

UPENDEZI wa watu wengi huamshwa na fumbo​—hadithi yenye utatanishi, yenye vidokezi vinavyoweza kueleweka kwa njia mbalimbali, na yenye mwisho wa kushangaza, labda kupata hazina fulani. Ikiwa upendezi wako wewe huamshwa, wewe utafurahia ‘Lile Fumbo la Malango.’

Fumbo hili lilianza kutokeza wazi kule Megiddo, jiji lililo katika mahali penye mafaa makubwa lililokuwa ndilo pitio kubwa la njia za kibiashara na kijeshi katika Mashariki ya Kati. Wachimbuzi wa vitu vya kale walifukua mabaki ya lango moja la ulinzi linalostahili kufanyiwa ukumbusho, ambalo ithibati yenye kupatikana iliwasadikisha kwamba lilikuwa la kutoka wakati wa Mfalme Sulemani. Lilikuwa na ufanano gani? Hapo ndipo vidokezi vilianza.

Tazama kile kiolezo cha Megiddo ya kale upande wa kuume, na hasa kwenye eneo la lango ambalo limekaziwa zaidi. Msafiri ye yote wa kale au jeshi lo lote la ushambulizi lenye kuipanda barabara ya kwenda kwenye jiji hilo lenye ngome alifika kwanza kwenye lango la mbele. Upande wa ndani mlikuwa na kitalu kikubwa, au ua. Humo washambulizi wo wote wangeonekana wazi walipokuwa wakisogea mbele na kugeukia kushoto ili wafikie lile lango kuu la ulinzi, ambalo ndilo lililo katika kiini cha fumbo letu.

Minara yenye ngome ilifanyiza pande za mbele za lango hilo. Muundo wa lango zima ulijengwa, si kwa jiwe au tofali la kikawaida la kondeni, bali kwa mawe ya mraba yaliyochongwa kwa uangalifu ambayo yalikuwa asili ya kipindi cha Sulemani. Lakini kulikuwa na mtindo wa upambanufu ndani ya lango hilo. Katika pande za sebule ndefu kulikuwa na nguzo kubwa za kushikilia, ambazo zilifanyiza vyumba sita ambapo walinzi wangeweza kukaa. (Linganisha Ezekieli 40:6, 10, 20, 21, 28, 29.) Katika nyakati zilizo za kikawaida, gari-farasi au kikundi cha wafanya biashara kingeweza kupita kwa urahisi, hata hivyo mambo yangekuwa mengine kwa wa-shambulizi walioweza kugonga na kubomoa ile milango mikubwa mizito na kupita. Zile nguzo zingelazimisha washambulizi waingie katika kipitio chembamba, wapite mbio hapo wakichapwa-chapwa kweli kweli na wanaume wenye silaha wa jeshi la Megiddo, lililowazunguka pande zote katika vyumba vya kuume na kushoto.

Sasa lile fumbo linahama na kwenda kaskazini mwa Bahari ya Galilaya kwenye kilima, au chungu, cha Hazori ya kale, ambako Profesa John Garstang alikuwa amefanya uchimbuzi katika 1928. Yigael Yadin mchimbuzi Mwisraeli wa vitu vya kale aligeuka kwenda kwenye kilima hiki kikubwa sana katika 1955. Yeye alikuwa akifikiria taarifa moja ya Kibiblia inayosomwa hivi: “Huu ndio usimulizi wa wale walioandikishwa kwa ajili ya kazi ya lazima ambayo Mfalme Sulemani alishurutisha ili kujenga nyumba ya Yehova na . . . ukuta wa Yerusalemu na Hazori na Megiddo na Gezeri.” (1 Wafalme 9:15, NW) Lilionekana kuwa jambo la kiakili kwamba wahandisi wa Sulemani wangefuata ramani fulani iliyo kuu kwa ajili ya ngome kama hizo katika majiji mengineyo waliyojenga. Je! malango hayo ya Kisulemani yalikuwako Hazori?

Kadiri ambavyo wafanya kazi wa Yadini walifanya maendeleo katika uchimbuzi wao, walipata ukuta maradufu wenye vyumba katikati vilivyozungushiwa ngome juu. Ndipo muundo mkubwa wenye kukamatana na kuta hizo ukaanza kuonekana. Yadin anasema: “Mara hiyo sisi tukang’amua kwamba tulikuwa tumegundua lile lango . . . Zaidi ya hilo, baada ya muda mfupi ilikuwa wazi kwamba muundo wa ujenzi wa lango hilo​—lililokuwa na vyumba sita na minara miwili​—na pia marefu na mapana yalo yalikuwa sawa na yale ya lango lililogunduliwa [miaka mingi] mapema kule Megiddo . . . Taharuki iliongezeka sana katika kambi yetu . . . Tulichora-chora katika ardhi ule muundo wa lango la Megiddo, tukitia alama kwa kutumia vigingi ili kuonyesha sehemu za pembeni na za kuta, halafu tukaagiza wafanya kazi wetu wachimbe kulingana na ule utiaji-alama, tukiahidi hivi: ‘hapa mtapata ukuta,’ au ‘pale mtapata chumba kimoja.’ ‘Manabii’ yetu yalipothibitika kuwa sahihi, fahari yetu iliongezeka ajabu . . . Tuliposoma mstari ule wa kibiblia [ili wao wasikie] juu ya utendaji mbalimbali wa Sulemani katika Hazori, Megiddo na Gezeri, fahari yetu ilishuka chini kwa haraka, lakini ile ya Biblia ikainuka juu kabisa!”​—Hazor: The Rediscovery of a Great Citadel of the Bible.

Ilionekana kama kwamba lile fumbo la malango lilikuwa linatatuliwa kabisa kabisa kama ilivyotarajiwa kulingana na vidokezi katika Biblia. Hata hivyo, namna gani juu ya Gezeri, upande wa kusini? Yadin alijua kwamba R. A. S. Macalister, mchimbuzi Mwailandi wa vitu vya kale ambaye alikuwa amechimbua huko kati ya 1902 na 1909, hakupata kitu cho chote chenye kuhusishwa na Sulemani. Je! ingeweza kuwa vidokezo vya maana vilikuwa vimekosa kuonwa katika lile ambalo hata Yadin aliliita “Fumbo la Gezeri”?

Yeye anasimulia hivi: “Magunduzi kule Hazor na kile kifungu cha maneno yenye sifa sana katika 1 Wafalme yaliniongoza kwenye uchunguzi mpya kabisa wa ripoti ya Macalister kwa tumaini la kupata lango moja. Mmoja anaweza kuwazia mduwao wangu na taharuki isiyo na mipaka wakati . . . nilipokuja kwenye mchoro fulani. . . wenye kichwa ‘Ramani ya Husuni ya Kimakabayo ya Gezeri.’” Macalister alionyesha tarehe ya mabaki ya “husuni” (ngome) hiyo kuwa ya wakati wa uasi wa Wamakabayo Wayahudi (karne ya pili K.W.K.). Lakini Yadin aliwaza kwamba angeweza kuona katika mchoro huu wa zamani ‘ukuta maradufu wenye vyumba kati-kati vilivyozungushiwa ngome juu, nyumba-lango ya nje-nje, na la maana hata zaidi, kitu ambacho kilifanana na nusu ya lango la jiji sawasawa kabisa na vile ambavyo vilipatwa katika Megiddo na Hazori.’ Yadin alitangaza makala moja juu ya vidokezo hivi. Baadaye, Dakt. William G. Dever alichimbua kule Gezeri. Tokeo likawa nini? Dever aliandika hivi kwa taharuki: “Kweli kweli Sulemani alijenga upya Gezeri!” Au kama vile Yadin anavyoweka maneno hayo; “Kwa uhakika kabisa, si kwamba tu kikoa cha Dever kilipata ile nusu nyingine ya lango, bali pia ule mpangilio wa mawe na udongo uliotumiwa kujengea ulionyesha kwa kukata shauri kwamba huo mjengo-tata ulikuwa umejengwa nyakati za Sulemani.”

Kwa hiyo lile fumbo lilifumbuliwa. Yadin alionelea hivi katika The Biblical Archaeologist (Buku 33, 1970, 3): “Kwa msaada wa kile kifungu kifupi cha maneno ya kibiblia kutokana na Wafalme, zile ngome za Kisulemani, zenye kufanana kabisa katika ramani ya mchoro wazo katika yale majiji matatu, zilipatikana na kuwekewa tarehe zinazohusiana nazo.” “Kweli kweli, inaonekana kwamba hakuna kielelezo cho chote katika historia ambapo kifungu cha maneno kimesaidia sana kutambulisha na kujua tarehe za miundo iliyo katika vilima kadhaa kati ya vile vilivyo vya maana zaidi . . . kama vile ambavyo 1 Wafalme 9:15 imesaidia.”

[Picha katika ukurasa wa 25]

Kwa kutegemea 1 Wafalme 9:15, wachimbuzi wa vitu vya kale walipata kule Hazori lango moja lenye ukubwa na umbo lililo kama lile lililo katika Megiddo

[Picha katika ukurasa wa 26]

Mwono wa kutoka angani wa lango lililoko Gezeri. Mchoro huu unaonyesha kilichofukuliwa kwanza (kwenye mstari kamili ulioshikamana) na kilichopatwa yapata miaka 60 baadaye (kwenye mstari wa vitone-tone)

[Credit Line]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Picha Credit Line katika ukurasa wa 24]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki