-
Alivumilia Licha ya Ukosefu wa HakiMnara wa Mlinzi—2014 | Februari 1
-
-
Tunaposoma kuhusu njama yake, tunashangaa kuona jinsi alivyokuwa mwovu. Malkia Yezebeli alijua kwamba Sheria ya Mungu ilitaka ushahidi wa watu wawili ili kuthibitisha makosa mazito. (Kumbukumbu la Torati 19:15) Basi, akaandika barua kwa jina la Ahabu, akiwaagiza wanaume wenye vyeo wa Yezreeli watafute wanaume wawili ambao wangetoa mashtaka ya uwongo dhidi ya Nabothi, kwamba alikuwa amekufuru, kosa ambalo adhabu yake ilikuwa kifo. Kwa kusikitisha, njama yake ilifaulu. Wanaume wawili “wasiofaa kitu” walitoa ushahidi wa uwongo dhidi ya Nabothi, na akapigwa mawe hadi akafa. Isitoshe, wana wa Nabothi waliuawa pia!b (1 Wafalme 21:5-14; Mambo ya Walawi 24:16; 2 Wafalme 9:26) Ahabu alikuwa amepuuza majukumu yake na kumruhusu mkewe afanye alivyotaka kwa kuangamiza watu wasio na hatia.
-
-
Alivumilia Licha ya Ukosefu wa HakiMnara wa Mlinzi—2014 | Februari 1
-
-
b Kama Yezebeli aliogopa shamba hilo la mizabibu lingepewa warithi wa Nabothi, basi huenda hilo ndilo lililomchochea kupanga wana wa Nabothi wauawe. Ili kujua kwa nini Mungu anaruhusu ukandamizaji, soma makala “Wasomaji Wetu Wanauliza” katika gazeti hili.
-