-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Jambo hilo lilimkasirisha sana Hamani. Lakini hangetosheka kwa kumwangamiza Mordekai peke yake. Alitaka kuwaangamiza watu wote wa Mordekai! Hamani alizungumza na mfalme na kufanya Wayahudi waonekane kuwa watu wabaya. Bila kuwataja Wayahudi moja kwa moja, alisema wao si watu wa maana na kwamba “wa[me]tawanyika na kujitenga kati ya vikundi vya watu.” Hata alisema kwamba hawakuheshimu sheria za mfalme; hivyo, walikuwa waasi hatari. Kisha, akajitolea kuchanga kiasi kikubwa cha pesa kwa hazina ya mfalme ili kulipia kazi ya kuwaua Wayahudi wote katika milki hiyo.c Basi Ahasuero akampa Hamani pete yake ya kifalme ya mhuri ili atie mhuri amri yoyote aliyotaka itekelezwe.—Esta 3:5-10.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
c Hamani alitoa mchango wa talanta 10,000 za fedha, kiasi ambacho leo ni sawa na mamilioni ya dola. Ikiwa Ahasuero alikuwa Shasta wa Kwanza, basi huenda pesa hizo zilimchochea akubali pendekezo la Hamani. Shasta alikuwa ametumia pesa nyingi sana alipopigana na Wagiriki katika vita vilivyosababisha uharibifu mkubwa. Labda alipigana vita hivyo kabla ya kumwoa Esta.
-