Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 20 “BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami? nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga; nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka; niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako; nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.”—Isaya 44:24-28.

  • Mungu wa Kweli Anatabiri Ukombozi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 22. Eleza Mto Eufrati unakauka jinsi gani.

      22 Kwa kawaida waaguzi wasiopuliziwa hawathubutu kutabiri mambo hususa, kwa kuhofu kwamba watathibitishwa kuwa waongo baada ya muda. Lakini Yehova ni tofauti kwa sababu anafunua kupitia Isaya jina hususa la mwanamume ambaye Yeye atamtumia kuwaweka huru watu wake watoke utekwani, waweze kwenda nyumbani wakajenge upya Yerusalemu na hekalu. Jina lake ni Koreshi, na anajulikana kuwa Koreshi Mkuu wa Uajemi. Yehova anatoa hata maelezo madogo-madogo kuhusu maarifa ambayo Koreshi atatumia kuupenya mfumo mkubwa sana wa Babiloni ulio na kinga nyingi. Babiloni italindwa na kuta ndefu na mapito ya maji yanayotiririka ndani ya jiji na vizingo vyake. Koreshi atageuza sehemu kubwa ya mfumo huo—ule Mto Eufrati—itimize lengo lake. Kulingana na wanahistoria wa kale Herodotus na Xenophon, katika upande fulani wa juu wa Babiloni, Koreshi aliyaelekeza kando maji mengi ya Mto Eufrati maji yakapungua kiasi cha askari zake kupita kwa miguu. Eufrati unakauka kwa maana ya kwamba hauwezi kulinda Babiloni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki