Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Faraja kwa Watu wa Mungu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 12. Kwa nini watumishi wa Mungu hawapaswi kuogopa wanapoharibiwa jina na wapinzani wa kibinadamu?

      12 Sasa Yehova anaongea na watu wale ‘wanaofuatia uadilifu,’ akisema hivi: “Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao. Maana nondo itawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote.” (Isaya 51:7, 8) Wale wanaomtumainia Yehova wataharibiwa jina na kusutwa kwa sababu ya msimamo wao wa ushujaa, lakini hilo si jambo la kuogopwa. Wasutaji ni wanadamu tu wenye kufa, ambao ‘wataliwa,’ sawa na vile vazi la sufu huliwa na nondo.a Kama vile Wayahudi waaminifu wa kale, Wakristo wa kweli leo hawana sababu ya kuwaogopa wapinzani wowote. Yehova, Mungu wa milele, ndiye wokovu wao. (Zaburi 37:1, 2) Suto kutoka kwa adui za Mungu ni ushuhuda wa kwamba watu wa Yehova wana roho yake.—Mathayo 5:11, 12; 10:24-31.

  • Faraja kwa Watu wa Mungu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Kulingana na ushuhuda, nondo anayetajwa hapa ni yule nondo mtengeneza-utando katika nguo, akiwa hasa katika ile hatua ya kuwa buu lenye uharibifu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki