Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 10. Ni matukio gani yanayotoa ishara ya mambo mabaya kwa jiji?

      10 Isaya afafanua hali inayobadilika: “Ikawa mabonde yako mateule yamejaa magari ya vita, nao wapandao farasi wamejipanga wakielekea malango. Kisha alikiondoa kifuniko cha Yuda.” (Isaya 22:7, 8a) Magari na farasi zajaa kwenye nyanda nje ya jiji la Yerusalemu nazo zajiandaa kushambulia malango ya jiji. “Kifuniko cha Yuda” kinachoondolewa ni nini? Huenda ni lango fulani la jiji hilo, ambalo kutekwa kwake ni ishara ya mabaya kwa walinzi.c Kifuniko hicho chenye ulinzi kiondolewapo, jiji labaki wazi ili washambuliaji waingie.

  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 11, 12. Wakazi wa Yerusalemu wachukua hatua zipi za kujilinda?

      11 Isaya sasa akaza fikira kwenye majaribio ya watu ya kujilinda. Wanachofikiria kwanza ni silaha! “Nawe siku hiyo ulivitazama vyombo vya vita katika nyumba ya mwituni. Nanyi mlipaona mahali palipobomoka katika mji wa Daudi ya kuwa ni pengi, nanyi mliyakusanya maji ya birika la chini.” (Isaya 22:8b, 9) Silaha zimewekwa katika ghala ya silaha kwenye nyumba ya mwituni. Solomoni ndiye aliyeijenga ghala hiyo ya silaha. Kwa kuwa ilijengwa kwa mierezi kutoka Lebanoni, ilikuja kuitwa “nyumba ya mwitu wa Lebanoni.” (1 Wafalme 7:2-5) Mahali palipobomoka ukutani pachunguzwa. Maji yakusanywa—hatua muhimu ya kujilinda. Watu hao wanahitaji maji ili kuishi. Pasipo maji, jiji haliwezi kudumu. Hata hivyo, ona kwamba haitajwi popote kuwa wanamtegemea Yehova ili kupata ukombozi. Badala yake, wanazitegemea njia zao wenyewe. Na tusifanye kamwe kosa kama hilo!—Zaburi 127:1.

  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • c Au, huenda usemi “kifuniko cha Yuda” warejezea kitu kingine tofauti kinacholinda jiji, kama vile ngome ambazo ni hifadhi za silaha na makao ya wanajeshi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki