-
‘Hapana Amani kwa Wabaya’Mnara wa Mlinzi—1987 | Julai 1
-
-
7. (a) Tunajuaje kwamba kuna kiwango kikubwa cha roho isiyoonekana kwenye mambo ya kibinadamu? (b) Hapo awali, ni nani waliokuwa mfalme wa kaskazini na mfalme wa kusini, na ushindani wao ulianzaje?
7 Kwanza malaika huyu anaeleza jinsi yeye, akiungwa mkono na Mikaeli, alikuwa amekuwa akipigana dhidi ya ‘wana-wafalme’ wa roho wa Ajemi na Ugiriki. (Danieli 10:13, Dan 10:20–11:1, NW) Ono hili fupi kwenye makao ya kiroho linathibitisha kwamba mapambano ya kitaifa yanatia ndani zaidi ya binadamu wa vivi hivi. Kuna majeshi ya kishetani, au “wana-wafalme,” wanaounga mkono watawala wa kibinadamu wenye kuonekana. Lakini tangu nyakati za kale, watu wa Mungu wamekuwa wakiwa na “mwana-mfalme,” Mikaeli, kuwatia nguvu dhidi ya mamlaka hizi za kishetani. (Waefeso 6:12) Ndipo malaika huyo anapoelekeza fikira zetu kwenye ushindani kati ya Siria na Misri. Yeye anaanza hivi: “Na mfalme wa kusini atakuwa hodari, na mmoja wa wakuu [“wana-wafalme,” NW] wake.” (Danieli 11:5a) Mfalme wa kusini hapa alikuwa Tolemi wa Kwanza, mtawala wa Misri, aliyeteka Yerusalemu karibu 312 K.W.K. Kisha malaika yule anaelekeza kwa mfalme mwingine ambaye “atakuwa hodari kuliko yeye, naye atakuwa na mamlaka; mamlaka yake itakuwa mamlaka kubwa [kuliko uwezo wa kutawala wa huyo mmoja, NW].” (Danieli 11:5b) Huyo ni yule mfalme wa kaskazini akiwa mtu Seleuko wa Kwanza Nikato, ambaye ufalme wake, Siria, ukawa wenye nguvu zaidi ya Misri.
-
-
‘Hapana Amani kwa Wabaya’Mnara wa Mlinzi—1987 | Julai 1
-
-
[Ramani/Picha katika ukurasa wa 12]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Bahari ya Kubwa
Siria
Uyahudi
Misri
-