-
“Mfalme wa Kaskazini” Katika Wakati wa MwishoMnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Mei
-
-
8. Ni nani ambaye amekuwa mfalme wa kusini katika kipindi chote cha siku za mwisho?
8 Wakati wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, serikali ya Marekani na Uingereza ziliungana na kufanyiza jeshi lenye nguvu nyingi sana. Wakati huo, Uingereza na koloni lake la zamani, Marekani, ziliungana na kutokeza Serikali Kuu ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani. Kama Danieli alivyotabiri, serikali hiyo ilikuwa imejikusanyia “jeshi kubwa kupita kiasi, tena lenye nguvu.” (Dan. 11:25) Katika kipindi cha siku za mwisho, muungano wa Uingereza na Marekani umekuwa ndio mfalme wa kusini.c Hata hivyo, ni nani aliyechukua nafasi ya mfalme wa kaskazini?
MFALME WA KASKAZINI AIBUKA TENA
9. Mfalme wa kaskazini aliibuka tena lini, na andiko la Danieli 11:25 lilitimizwaje?
9 Katika mwaka wa 1871, mwaka mmoja baada ya Russell na wenzake kuanzisha kikundi cha kujifunza Biblia, mfalme wa kaskazini aliibuka tena. Mwaka huo, Otto von Bismarck alichangia kwa kiwango kikubwa kuanzishwa kwa Milki ya Ujerumani. Mfalme Wilhelm wa Kwanza wa Prussia akawa maliki wa kwanza wa milki hiyo, naye akamteua Bismarck kuwa waziri mkuu wa kwanza.d Katika miaka iliyofuata, Ujerumani ikawa serikali ya kikoloni ikitawala nchi za Afrika na nchi zilizo kwenye Bahari ya Pasifiki, na ikaanza kupambana na Uingereza ili kupata mamlaka zaidi. (Soma Danieli 11:25.) Milki ya Ujerumani iliunda jeshi lenye nguvu nyingi sana na jeshi lake la majini lilikuwa la pili kwa ukubwa duniani. Ujerumani ilitumia majeshi hayo kushambulia maadui wake katika Vita vya Kwanza vya Ulimwengu.
10. Andiko la Danieli 11:25b, 26 lilitimizwaje?
10 Kisha Danieli anatabiri kuhusu kile kitakachoipata Milki ya Ujerumani na jeshi lake. Unabii huo unasema kwamba mfalme wa kaskazini “hatasimama.” Kwa nini? “Kwa sababu watapanga njama dhidi yake. Na wale wanaokula vyakula vyake bora watasababisha aanguke.” (Dan. 11:25b, 26a) Katika siku za Danieli, wale waliokula “vyakula bora ambavyo [mfalme] mwenyewe alikula” walitia ndani maofisa wa mfalme ‘waliomtumikia mfalme.’ (Dan. 1:5) Unabii huo unazungumza kuhusu nani? Unawahusu maofisa wa vyeo vya juu wa Milki ya Ujerumani—kutia ndani majenerali na washauri wa mambo ya kijeshi wa maliki—ambao hatimaye walipindua utawala wa maliki wa Ujerumani.e Unabii wa Danieli haukutabiri tu kuhusu kuanguka kwa milki hiyo, bali pia unataja matokeo ya vita kati ya mfalme wa kaskazini na wa kusini. Unabii huo unasema hivi kuhusu mfalme wa kaskazini: “Na jeshi lake litafagiliwa mbali, na wengi watauawa.” (Dan. 11:26b) Kama ilivyotabiriwa, jeshi la Ujerumani ‘lilifagiliwa mbali’ katika Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, na watu wengi ‘waliuawa.’ Watu wengi sana walikufa katika vita hivyo kuliko vita vingine vyovyote kabla ya hapo.
-
-
“Mfalme wa Kaskazini” Katika Wakati wa MwishoMnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Mei
-
-
e Walifanya mambo mengi yaliyosababisha milki yao ianguke haraka. Kwa mfano, waliacha kumsaidia maliki, walivujisha siri kuhusu habari nyeti za vita, na kumlazimisha maliki ajiuzulu.
-