-
Kitabu Cha Biblia Namba 32—Yona“Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
-
-
5. Yona aitikiaje mgawo wake, na tokeo ni nini?
5 Yona apewa mgawo kwenda Ninawi, lakini akimbilia mbali (1:1-16). “Basi neno la BWANA [Yehova, NW] lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.” (1:1, 2) Je! Yona apendezwa sana na mgawo huo? Hata kidogo! Yeye akimbilia mbali kuelekea upande ule mwingine, akipanda meli ya kwenda Tarshishi, yawezekana ni Hispania. Meli ya Yona yakutana na dhoruba kubwa. Kwa kuhofu mabaharia waitisha msaada, “kila mtu akamwomba mungu wake,” huku Yona akiwa amelala katika ngama ya meli. (1:5) Baada ya kuamsha Yona, wao watupa kura kwa jaribio la kugundua ni nani wa kulaumika kwa mashaka yao. Kura yaangukia Yona. Sasa ndipo yeye anapowajulisha kwamba yeye ni Mwebrania, mwabudu wa Yehova, na kwamba akimbilia mbali kutoka kwenye furushi lake alilopewa na Mungu. Awaalika wamvurumishe ndani ya bahari. Baada ya kufanya jitihada zaidi za kusalimisha meli dhorubani, mwishowe wamtupa Yona kutoka melini. Bahari yaacha fujo.
-
-
Kitabu Cha Biblia Namba 32—Yona“Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
-
-
9. Ni mtazamo na mwendo gani wa Yona wapasa kutokeza kuwa onyo kwetu?
9 Mwendo wa kutenda wa Yona na matokeo yao wapasa kutokeza kuwa onyo kwetu. Yeye alikimbia mbali kutoka kwa kazi aliyopewa na Mungu; yeye angalipaswa kujishughulisha na kazi hiyo na kutumainia Mungu amtegemeze. (Yona 1:3; Luka 9:62; Mit. 14:26; Isa. 6:8) Alipochukua hatua ya kwenda upande usiofaa, yeye alionyesha mtazamo usiofaa kwa kushindwa kujitambulisha waziwazi kwa mabaharia kuwa yeye ni mwabudu wa “BWANA [Yehova, NW], Mungu wa mbingu.” Alikuwa amepoteza ujasiri wake. (Yona 1:7-9; Efe. 6:19, 20) Kujifikiria kwa Yona kulimwongoza atetee heshima yake kwa kumwambia Yehova kwamba muda wote huo alijua kwamba hayo ndiyo yangekuwa matokeo—kwa hiyo ya nini kumpeleka akiwa nabii? Yeye alikaripiwa kwa ajili ya mtazamo huo usio wa staha, wa kulalamika, kwa hiyo twapaswa kunufaika na yaliyompata na kujiepusha na kutafutia kosa uonyeshaji rehema wa Yehova au njia yake ya kufanya mambo.—Yona 4:1-4, 7-9; Flp. 2:13, 14; 1 Kor. 10:10.
-