Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Utakwazika kwa Sababu ya Yesu?
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2021 | Mei
    • 3 Yesu alijua kwamba watu wengi wangekataa kukubali kwamba yeye ndiye Masihi. (Yoh. 5:39-44) Aliwaambia hivi wanafunzi wa Yohana Mbatizaji: “Mwenye furaha ni mtu ambaye hapati ndani yangu sababu ya kukwaza.” (Mt. 11:2, 3, 6) Kwa nini watu wengi walimkataa Yesu?

  • Je, Utakwazika kwa Sababu ya Yesu?
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2021 | Mei
    • (1) MALEZI YA YESU

      Filipo akimtia moyo Nathanaeli akutane na Yesu ambaye ameketi jirani.

      Watu wengi walikwazika kwa sababu ya malezi ya Yesu. Jambo hilo linaweza kuwakwazaje watu leo? (Tazama fungu la 5)b

      5. Kwa nini huenda baadhi ya watu walifikiri kwamba Yesu hakuwa Masihi aliyetabiriwa?

      5 Watu wengi walikwazika kwa sababu ya malezi ya Yesu. Walikubali kwamba Yesu alikuwa mwalimu mzuri na kwamba alifanya miujiza. Lakini machoni pao, alikuwa tu mwana wa seremala maskini. Na alitoka Nazareti, mji ambao ulionekana si muhimu. Hata Nathanaeli ambaye alikuja kuwa mwanafunzi wa Yesu, mwanzoni alisema hivi: “Je, kitu chochote kizuri kinaweza kutoka Nazareti?” (Yoh. 1:46) Huenda Nathanaeli hakuupenda mji ambao Yesu aliishi wakati huo. Au huenda alikuwa akikumbuka unabii unaopatikana katika Mika 5:2, ambao ulitabiri kwamba Masihi angezaliwa Bethlehemu, na si Nazareti.

      6. Ni jambo gani ambalo lingewasaidia watu katika siku za Yesu kutambua kwamba Yesu alikuwa Masihi?

      6 Maandiko yanasema nini? Nabii Isaya alitabiri kwamba maadui wa Yesu wangeshindwa kujishughulisha “na habari za kizazi [cha Masihi].” (Isa. 53:8) Habari nyingi kumhusu Masihi zilikuwa zimetabiriwa. Ikiwa watu hao wangekuwa wametenga wakati ili kupata habari kamili, wangetambua kwamba Yesu alizaliwa Bethlehemu na kwamba alikuwa uzao wa Mfalme Daudi. (Luka 2:4-7) Hivyo, Yesu alizaliwa mahali ambapo palitabiriwa katika Mika 5:2. Basi tatizo lilikuwa nini? Watu walifanya uamuzi haraka. Hawakuwa na habari kamili. Kwa sababu hiyo, walikwazika.

  • Je, Utakwazika kwa Sababu ya Yesu?
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2021 | Mei
    • (2) YESU ALIKATAA KUFANYA MIUJIZA ILI KUJIONYESHA

      Yesu akizungumza na umati wa watu.

      Watu wengi walikwazika kwa sababu Yesu alikataa kufanya ishara za kujionyesha. Jambo hilo linaweza kuwakwazaje watu leo? (Tazama fungu la 9 na 10)c

      9. Ni nini kilichotokea Yesu alipokataa kuonyesha ishara kutoka mbinguni?

      9 Baadhi ya watu katika siku za Yesu hawakuridhika na uwezo wake wa pekee wa kufundisha. Walitaka mengi zaidi. Walisisitiza athibitishe kwamba alikuwa Masihi kwa kuwaonyesha “ishara kutoka mbinguni.” (Mt. 16:1) Huenda walisisitiza jambo hilo kwa sababu hawakuelewa maana ya andiko la Danieli 7:13, 14. Hata hivyo, haukuwa wakati wa Yehova kutimiza unabii huo. Mambo ambayo Yesu alikuwa anafundisha yalitosha kuwathibitishia kwamba yeye ndiye aliyekuwa Masihi. Lakini alipokataa kuonyesha ishara waliyotaka, walikwazika.—Mt. 16:4.

      10. Yesu alitimizaje jambo ambalo Isaya aliandika kuhusu Masihi?

      10 Maandiko yanasema nini? Nabii Isaya aliandika hivi kumhusu Masihi: “Hatalia kwa sauti wala kupaza sauti yake, naye hatafanya sauti yake isikike barabarani.” (Isa. 42:1, 2) Yesu alifanya huduma yake bila kujionyesha. Hakujenga mahekalu na hakuvaa mavazi ya kidini yaliyomtofautisha na wengine au kuitwa kwa majina ya cheo ya kidini. Wakati wa kesi yake, Yesu alikataa kumpendeza Mfalme Herode kwa kufanya muujiza kwa ajili yake, ingawa maisha yake yalikuwa hatarini. (Luka 23:8-11) Yesu alifanya miujiza kadhaa, lakini kazi yake kuu ilikuwa kuhubiri habari njema. Aliwaambia hivi wanafunzi wake: “Nilikuja kwa kusudi hilo.”—Marko 1:38.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki